header

nmb

nmb

Saturday, February 15, 2014

WAKAZI WA JIJI LA MWANZA KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY KWA STYLE YA KIPEKEE.

 Mmoja wa Wakurugenzi wa Skylight beach Haruna Said akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza kuhusiana na matayarisho ya Burudani ya kipekee ya Valentine's day na Fullmoon Party litakalofanyika kwenye ufukwe wa ziwa Victoria, Skylight Beach Resort Malimbe jijini Mwanza. 
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa kabla ya ufunguzi wa Ukumbi wa burudani wa Disko kuanza wamejipanga kuanza kutoa burudani ya ufukweni maarufu Foolmoon Beach Part ambayo itakuwa inafanyika kila mwezi mara moja kwa lengo la kutambulisha bidhaa mbalimbali zitakazopatikana Skylight Beach Resort.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Syklight Group Ltd, ‘Jembe ni Jembe’ Innocent Maletho (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza kutambulisha burudani zitakazo kuwepo usiku wa Valeentine pande za Skylight Beach Resort Malimbe jijini Mwanza.

Alisema kuwa katika siku hii ya shangwe kwa wakazi wa Rock city, kututakuwa na burudani mbalimbali toka kwa MAdj wakali,  DVJ Frank,  DVJ Denis na DVJ Davy ambao watatambulisha mfumo mpya wa burudani ya kiwango cha kimataifa. Pia tutakua na Dj mgeni (Guest DJ),kutoka Dar es salaam, DVJ MAFUVU Atakayedondosha ngoma kali kwa watakao hudhuria.

Wandishi wa habari wakijadiliana juu ya tukio hilo huku wakiweka kumbukumbu kwa yale yanayopaswa kuwafikia walaji wa habari aka jamii.
Kona ya wanahabari.
Baadhi ya wadau wa Skylight Beach Resort Mwanza wakiweka mambo sawa kubainisha huduma zitakazo kuwa zikitolewa kwenye kiota hicho kipya chenye hadhi ya kitalii nchini. Kutoka kushoto ni meneja masoko wa Skylight Beach Resort, Ombeni Charles, Afisa masoko Innocent Maletho, mmoja kati ya wakurugenzi wa 'Jembe ni Jembe' Haruna Said, Dvj Frank na Mdau wa kitengo cha huduma vinywaji Skylight Beach Resort Mwanza.  
Meneja Ubunifu Matukio wa Skylight Beach Resort Albert G. Sengo (Pichani) amesema kuwa ujio wa Skylight Beach Resort umekuja kwa nia ya kuitikia wito wa Serikali ya Mkoa wa Mwanza kwa wadau wake wazalendo na wageni kuwekeza katika jiji hilo kwa nia ya kukuza Sekta ya Utalii sambamba na uboreshaji wa huduma za mahoteli Kanda ya Ziwa. 
Mkare Front Bar ni mmoja kati ya maeneo ya kiota hicho cha Skylight Beach Resort Mwanza, kitakacho tambulishwa ambapo Part hilo la Valentine linalo ambatana na tukio la Foolmoon Party litafanyika.
This is Skylight Beach Resort

No comments:

Post a Comment