header

nmb

nmb

Monday, February 1, 2010

Kumbe LIVERPOOL ni zao la EVERTON F. C!


LIVERPOOL ni moja
ya klabu Duniani na iliyo na historia yenye kuvutia
katika medani ya soka, ni miongoni mwa klabu kubwa
iliyomo katika "Big Four" kwa kipindi kirefu sasa.
Historia ya klabu hii ni yenye kuvutia kwa kuwa ni klabu
iliyotoka katika mifupa ya klabu ya Everton baada ya
mtafaruku kuzuka katika klabu hiyo (Everton) miaka ya
nyuma kabla ya kuzaliwa kwake.



Historia ya Liverpool
inaonesha kuwa, kuwepo kwa mfarakano wa ndani kwa ndani
katika Klabu ya Everton toka mwaka 1890 ulisababisha
baadhi ya wadau kuitema klabu hiyo na kuanzisha klabu
yao.







Mgogoro wa Everton, ulizuka kati ya kamati ya
klabu hiyo (Everton) na mmoja wa wadau wakuu, John
Houlding ambaye pia alikuwa rais wa klabu hiyo.
Pamoja
na Houlding kuwa mmilikiwa Everton, ndiyo aliyekuwa
mmiliki kiwanja maarufu sasa kiitwacho Anffield.




Kamati
ya Everton ilimtuhumu Houlding kuwa maamuzi yake katika
klabu hiyo yanasukumwa na mtazamo wa kisiasa na maslahi
binafsi kwa kuwa yeye ndiye alikuwa na maamuzi ya
mwisho.




Tabia hiyo ya kujiamulia atakacho katika klabu hiyo
ilizua utata na kufanya kundi kubwa katika klabu hiyo
kumchukia, maamuzi ya kumtimua Houlding yalikuwa magumu
kutokana na kuwa ndiye aliyeshika mizizi ya klabu hiyo
kipesa na kimadaraka.




Pamoja na hivyo, baadhi ya
wanankamati wa Everton waliamua kumwanzishia zengwe la
kumng'oa madarakani, walitaka kubadilishwa kwa mfumo wa
uongozaji klabu hiyo ili uwe na maslahi kwa kiwa
muhusika tofauti na alivyokuwa akitaka mmiliki huyo.
Mdudu wa chuki ukapanda kichwani mwa wadau hao, idadi ya
watu wanaompinga iliongezeka hivyo kujikuta akiwa na
kundi dogo linalomfuata, ni la wale "wapenda pesa."
Hali baadaye ilizidi kuwa mbaya ndani ya Everton na
hatimaye Houlding aliamua kubwaga manyanga.




Ikumbukwe
kuwa Anffield ilikuwa chini ya himaya ya yake, Everton
ilianza kuhaha baada ya kumtema Houlding, kutokana na
ukata uliokuwa ukiizonga Everton, baadhi ya wadau wa
klabu hiyo walishauriana na kuamua kupitisha mchango
kutoka katika tasisi mbalimbali ili kuiwezesha klabu
hiyo kusimama.




Karibu na uwanja wa Anffiel, kulikuwa na
eneo kubwa, Everton ilitaka kununua sehemu hiyo walau
iwe ikifanyia mazoezi yake lakini Houlding kutokana na
jeuri ya fedha alilinunua eneo hilo, hapo Everton
ilirudi nyuma.




Baada ya mambo kuwa magumu zaidi,
Everton iliamua kurudi kwa Houlding na kukodi uwanja
wake kwa ajili ya mazoezi na maandalizi ya mechi
mbalimbali.




Ili kuikomoa klabu hiyo, Houlding aliamua
kuongeza kodi kwa makusudi ambapo awali Everton ilikuwa
ikilipa pauni 100 na kuwa paun 250 kwa mwaka, kipindi
hicho kodi hii ilikuwa ni kubwa sana.




Kitendo hicho kilianza kuiyumbisha klabu hiyo kwa mara
nyingine lakini walijizatiti, ilikuwa mwaka 1890.
Hata
hivyo, baadaye Everton ilifanikiwa kununua sehemu
nyingine na kujenga uwanja wake huku Houlding akiwa
analalamikiwa na wadau wengi kutokana na tabia yake.
Awali Houlding alitaka kuwamilikisha uwanja huo Everton
lakini walimshtukia kuwa angeweza kuwazubaisha na
kushindwa kujenga uwanja wao.




Ilielezwa kuwa, faida
aliyokuwa akiipata Houlding katika biashara zake
ilimsukuma kutaka kuwapa tena uwanja ili aendelee
kuneemeka.




Baada ya kushindwa kwa mikakati yake,
Houlding aliamua kujing'atua akiwa na kundi dogo la
wapambe na kuanzisha klabu yake ambayo aliipa jila la
Everton Athletic, aliamua kuchagua rangi ile ile ya bluu
iliyokuwa ikitumiwa na Everton F.C. Kutokana na
ushawishi wake kifedha, jina hilo lilisajiliwa harakwa
Machi 15, 1892.




Kutokana na baadhi ya kanuni nchini
humo, Baraza la Soka la Uingereza liliigomea kuipa
kibali cha kucheza mechi kubwa klabu hiyo kutokana na
kukiuka baadhi ya masharti ikiwa ni pamoja na kutumia
rangi ya bluu bila kutofautisha hata kidogo na jezi za
Everton F.C.




Baraza hilo lilisema kuwa bado jina hilo
linaualakini, pia klabu hiyo kutokuwa na idadi kamili na
uongozi unaoeleweka. Houlding ili kumaliza mzizi wa
fitina, ndipo alipofikiri na kuamua kubadilisha jina
hilo na kuiita timu yake Liverpool, ilikuwa Juni
1892.




Everton ikiwa chini ya umiliki wa Houlding na
kabla ya kuzaliwa kwa Liverpool, ilicheza mechi yake ya
mwisho 18 Aprili 1892 dhidi ya Bolton Wanderers.
Houlding akiwa na kundi dogo la wapambe, aliamua
kumtafuta kocha wa klabu hiyo ambaye atatafuta nyota
wakali na hatimaye aendelee kuwa raisi wa klabu hiyo
mpya.




Ndipo alipoamua kumfuata John McKenna ili kuwa
mkurugenzi wa klabu yake, McKenna ndio mkurugenzi wa
kwanza wa Liverpool, ili kukisuka vizuri kikosi hicho,
McKenna kitu cha kwanza aliamua kwenda nchini Scotland
kusaka vipaji.




Nchini humo, alisaka wachezaji katika
klabu mbalimbali na hatimaye kuibuka na wachezaji 13
ambao awali walitosha kuanzisha kikosi kamili cha
Liverpool.




Kabla ya kuwa na kauli mbiu "Yuo Will Never
Work Alone" ya sasa, Liverpool ilitumia kauli mbiu yake
"the team of the Macs," sababu kubwa ya kubeba kauli
mbiu hiyo ni kutokana na sehemu kubwa ya wachezaji wa
klabu hiyo herufi zao za kwanza za majina yao yalikuwa
yakianzia na herufi "Mc".




Baada Liverpool kukamilika,
kwa mara ya kwanza kama Liverpool F.C, ilianza kujipima
ubavu na klabu ya Rotherham Town na kuibamiza 7-1, mechi
hiyo iliwapandisha ari wachezaji wa Liverpool.
Walipojiona wanaweza, waliandaa na kupeleka maombi yao
katika ngazi za juu ili kushiriki katika kchuano
mbalimbali nchini humo, mara kwa mara maombi yao
yalikuwa yakigonga mwaba.




Iliendelea kuomba mechi za
hiari na ndipo ilipokutana na (baba mzazi) Everton F.C
na kuifunga 1-0, ilikuwa mwaka 1893. Kipigo hicho
kiliilainisha Baraza la Soka nchini humo na hatimaye
kuruhusiwa kushiriki katika ligi mbalimbali nchini
humo.




Kuanzia hapo, Liverpool ilianza kushika kasi,
ilikuwa haikamatiki baada ya kuwa na tabia ya kuzibamiza
timbu mbalimbali ilizokutana nazo, baada ya muda mfupi,
ilitajwa kuwa timu tishio nchini humo, wakati huo
ilikuwa ikiongozwa kwa karibu na Tom Watson na kocha
mkuu alikuwa George Patterson.




Mwaka 1990, kocha
Patterson aliamua kubadilisha rangi ya jezi za klabu
hiyo kutoka bluu na kuwa nyeupe, na baadaye kuwa nyeupe
na nyekundu na hatimaye kutumia rangi nyekundu
inayotawala jezi mpaka sasa.




Baada ya kuipaisha na
kuanza kuipa heshima klabu hiyo, Patterson aliamua
kukabidhi madaraka kwa George Kay ambaye aliiongoza
klabu hiyo toka mwaka 1936 hadi 1951.




Patterson
alifanya hivyo baada ya kujiona amechoka kuiongoza klabu
hiyo, hata hivyo utawala wa Kay ulionekana kuwa dhaifu
na kuifanya klabu hiyo ianze kupoteza umaarufu.




Udhaifu
wake ulianza kuonekana katika mechi 12 za mwanzo, tatu
kati ya hizo alishinda na nne alitoka suluhu na zingine
kufungwa, mpaka kumalizika kwa msimu huo (1936/37),
Liverpool ilikuwa nafasi ya 14, msimu uliofuata
ilijinyanyua na kushika nafasi ya 11.




Ili kupoteza
mawazo, Liverpool baada ya kuisha kwa msimu huo, iliamua
kwenda kupunga upepo nchini Marekani na Kanada, kitu
ambacho kinaelezwa kuwa kiliongeza hamasa kwa wachezaji
wa klabu hiyo.




Kitendo cha Manchester United kuibamiza
Liverpool 5-0 katika msimu uliofuata, kilionekana
kuwaumiza sana wachezaji na mashabiki wake ambao
walikuwa wakiongezeka kila siku, hapo upinzani mkubwa wa
Liverpool na Manchester Unitedi ulianza.




Katika
historia ya klabu hiyo, meneja Kay ndio kiongozi wa
kwanza kuionekana kuwa na mafanikio mwishoni mwa utawala
wake, Januari 1956 Kay alibwaga manyanga katika klabu
hiyo kwa ridhaa yake.




Mikoba ya Kay ilichukuliwa na Don
Welsh kuanzia mwaka 1951 hadi 1956.
Welsh aliingia
katika mikono mibaya ya klabu hiyo kwa kuwa kipindi
hicho kulikuwa na matatizo ya hapa na pale, pamoja na
hivyo alijitahidi kufanya kila liwezekanalo na hatimaye
kukaa na klabu hiyo kwa miaka mitano tu.




Kutokana
maendeleo duni ya klabu hiyo, ilisababisha uongozi wa
klabu hiyo kumwachisha kazi na kumtafuta meneja mwingine
aliyeaminika kuwa na uwezo wa kuinua matumaini ya klabu
hiyo iliyokuwa tayari imejizolea umaarufu barani
humo.




Ndipo Phil Taylor alipochukua nafasi hiyo mwaka
1956. Taylor alifanya juhudi na kuiwezesha klabu hiyo
kushika nafasi ya nne katima msimu 1956/57 ambapo kila
mmoja alimkubali kutokana na mikakati yake, lakini
baadaye aliachia ngazi kutokana na kile alichokiita
majungu katika klabu hiyo.




Mikoba yake ilichukuliwa na
Bill Shankly, aliiongoza timu hiyo kuanzia 1959 hadi
1974, pia aliingia katika historia ya makocha walioiacha
klabu hiyo katika nafasi nzuri.




Ndani ya miaka 15 ya
uongozi wake, aliifanya klabu hiyo kuaminika kuwa klabu
bora na yenye kutisha Uingereza. Shankly na hatimaye
kufikia tamati ya uongozi wake mwaka 1974.




Bob Paisley
ndio mocha aliyefuata, alianzia mwaka 1974 hadi 1983,
naye moto wake ulikuwa mkali ingawa haikuwa sawa na
mtangulizi wake.
Baada ya Paisley, aliingia Joe Fagan
ambaye alidumu na klabu hiyo kwa miaka miwili yaani 1983
hadi 85 na kumpisha Kenny Dalglish ambaye naye
baliiongoza klabu hiyo kwa miaka sita (1985-1991) kisha
alimwachia Graeme Souness 1991 1994.




Souness
alionekana kuingia kwa mbwembwe katika uongozi wake,
ambapo kwa haraka alifanya maamuzi ya kuuuza baadhi ya
wachezaji walioonekana kuwa bora zaidi katika klabu
hiyo, aliwauza Ray Houghton na Steve Staunton ambapo
alitumia pesa nyingi kumnunua recklessly, Paul Stewart,
Torben Piechnik pamoja na Istvan Kozma.




Wachezaji hao
walikumbwa na kebbehi za mashabiki kwa kuwa walionekana
kutofanya chochote kipya katika klabu hiyo na kumfanya
Souness kuingia katika lawama kubwa.
Baada yake, mikoba
yake ilikamatwa na Roy Evans mwaka 1994 hadi 1998,
ambapo baada ya miaka minne alimpisha kocha Gérard
Houllier, ilikuwa ni mwaka 1998 hadi 2004 ambaye aliamua
kufanya kazi kwa kushirikiana na mchezaji wa zamani wa
Ufaransa Roy Evans, lakini Evans aliamua kujitoa.




Hapo
ndipo Rafael Benítez kocha wa sasa alipoamua kujitwika
mzigo wa kuionoa klabu hiyo mwaka 2004.
Mwaka jana 22,
Januari, Liverpool iliingia katika mtafaruku dhidi ya
mashabiki wake wakati wa mechi kati yake na Aston Villa,
mashabiki hao walitaka miongoni mwa wadau wa kuu wa
klabu hiyo akiwemo Gillett kuachana na klabu hiyo kwa
kuiuzia Liverpool hisa zao.



Hii ilitokana na wadau hao
kuwa na maamuzi ya mwisho katika kuiongoza klabu hiyo,
mashabiki hao walirudi nyuma katika historia ya uongozi
wa Bill Shankly kuwa hakutaka mwingiliano katika maamuzi
ya busara na yanayohitaji wa hali ya juu bila kuathiri
klabu, hakutaka mtu mwimgine amwingilie katika maamuzi
yake hivyo walimtaka Benitez kuwa mwamuzi wa mwisho kwa
kuwa ndio anayejua siri kubwa ya klabu.







Juni 4, 2007,
msemaji wa UEFA, William Gaillard alinakiliwa katika
vyombo vya habari nchini humo, akiwalaumu mashabikiwa
Liverpool kuwa na watu wa vurugu zinazoweza kuhatarisha
usalama wa watu wengine, vurugu hizo zilikuwa zikihusu
Gillett kuachana na klabu hiyo.







uwanja wao

No comments:

Post a Comment