Wednesday, March 21, 2012

Kamanda Gurdumo wa Msondo aebdelea Vizuri





Na Mwandishi Wetu

MWANAMUZIKI maarufu wa bendi kongwe ya Msondo ngoma, Muhidin Gurumo aliyelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ugojwa wa shinikizo la damu anaendelea vizuri.

Akizungumza na Dar es Salaam jana,Msemaji wa bendi hiyo Rajabu MHamila 'Super 'D' alisema afya Gurumo inaendelea vizuri na wakati wowowte anaweza kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo.

Alisema kuwa madaktari wanataka kuchukua vipimo vya mwisho kwa kina kujua kila kitu kinachop msumbua katika mwili wake.

"Kwa sasa tunashukuru Mungu afya ya Gurumo inaendelea vizuri tofauti na mara ya kwanza na akiendelea hivi anaweza hakurusiwa hivi karibuni"alisema Super D.

Hata hivyo aliwataka wapenzi wa bendi hiyo kumuombea duwa mwanamziki huyo ili apone upesi pia aliongeza kwa kusema maonesho yao ya wikii hii ni kama ifuatavyo Alhamisi watakuwa Mwandege Mkoa wa Pwani,Ijumaa watapiga katika viwanja vya Lidaz Clab jumamosi watakuwa katika viwanja vya TCC Sigara na Jumapili watamaliza wiki endi katika ukumbi wa Max Bar uliopo Ilala Bungoni.

DAR YAZIDI KUPENDEZA



Tuesday, March 20, 2012





JK AZINDUA UJENZI JENGO LA USHIRIKA TOWERS, DAR






Mchoro wa Jengo jipya la Ushirika Towers linalojengwa Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam

Rais Jakaya Kikwete akifunua pazia kuweka jiwe la mssingi wa ujenzi wa jengo hilo linalomilikiwa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC).


JK akikabidhiwa zawadi na Balozi wa China nchini, wakati wa hafala ya uzinduzi wa ujenzi wa jengo hilo linalojengwa na kampuni ya China

JK akizungumza na baadhi ya viongozi wa Taasisi za Fedha zilizoikopesha TFC kujenga jengo hilo

JK akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa TFC pamoja na wageni waalikwa

Wana Ushirika wakiwa na furaha walipokuwa wakiandamana mbele ya Rais Kikwete wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya mwaka wa Kimataifa wa Ushirika Duniani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo









Bendi ya DDC Mlimani Park, ikitumuiza wakati wa maadhimisho hayo. (PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA)





You might also like:

DIDA WA G" ATASIKIKA TENA RADIO TIMES 100.5


Baada ya kuweka mambo sawa..... takribani miezi mitatu sasa, napenda kuwajulisha ujio wangu mpya ndani ya Times 100.5 Fm



Tega sikio kama kawa kama dawa ktk frequency zilezile za Radio Times Fm kutokea Kawe Beach jijini DSM. Nitakuwa hewani na kipindi changu kilekile nilichokianzisha miaka nane iliyopita cha MITIKISIKO YA PWANI, na mishale ni ile ile Saa 6 mchana mpaka 10 jioni.



Wadau wa Dar na vitongoji vya karibu na Magomeni tutasomana ndani ya Traverntine Hotel ktk show kali ya Taarab na mduara jumapili ya Tar. 25 usiku



KIAFRIKA ZAIDI!

Thursday, March 15, 2012

Asha-Rose Migiro achelewesha Baraza jipya la Mawaziri





Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa UN, Dk. Asha- Rose Migiro.















Na Mwandishi wetu





NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Asha - Rose Migoro, anaelezwa kuwa sababu ya Rais Jakaya Kikwete kuchelewa kufanya mabadiliko katika Baraza lake jipya la Mawaziri, Gazeti Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Vyanzo vya habari kutoka serikalini vilisema kuwa Migiro ambaye ameomba kupumzika kuendelea na majukumu ya umoja huo kuanzia Juni mwaka huu ni mmoja kati ya watu wanaotegemewa na Rais Kikwete kuongoza moja ya wizara nyeti nchini.

“Rais kwa sasa yuko tayari kufanya mabadiliko kutokana na ukweli kwamba baadhi ya mawaziri wake wamechoka, wengine ni wagonjwa na wengine wanafikiria urais mwaka 2015. Kinachochelewesha mabadiliko hayo ni ujio wa Mama Migiro kwani hataki kufanya mabadiliko sasa, baada ya mwezi mmoja apangue tena kwa ajili ya kumuingiza Migiro,” kilisema chanzo chetu cha uhakika cha habari.

Sababu nyingine inayotajwa kucheleweshwa kwa mabadiliko katika Baraza la Mawaziri ni pamoja na kauli za shinikizo zinazotolewa na watu wa kada mbalimbali wakimtaka rais apangue baraza lake ili kumg’oa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda na Naibu wake, Lucy Nkya, kutokana na mgomo wa madaktari uliosababisha vifo vya Watanzania wengi.

Mbali na mawaziri hao, Rais Kikwete pia amekuwa akipata shinikizo la kuwaengua katika baraza lake mawaziri wanaougua kwa muda mrefu, akiwamo Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya.

“Rais Kikwete hawezi kufanya mabadiliko hayo kwa sasa kwani akifanya hivyo ataonekana amefanya kutokana na shinikizo. Kwa vyovyote vile madiliko hayatakuwepo kwa sasa hadi Juni baada ya kurejea Mama Migiro,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Hata hivyo haikuweza kujulikana mara moja Migiro atashika wizara gani, lakini habari zinasema kuwa ataongoza moja ya wizara nyeti nchini.

Wakati akiondoka nchini kwenda kushika nafasi hiyo UN, Migiro ambaye anatajwa kuwa mmoja wa watu wanaotarajiwa kuwania nafasi ya urais mwaka 2015, alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, alitangaza mabadiliko makubwa katika safu ya uongozi ndani ya Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa, ambapo alithibitisha kuwa Naibu Katibu Mkuu, Dk. Asha- Rose Migiro ameomba kupumzika. Vijar Nambiar ambaye ni Mkuu wa Ofisi yake (Chef de Cabinet), pia anaachia ngazi UN.

“Kama mlivyotangaziwa mwishoni mwa mwaka jana kuhusu mabadiliko yanayotarajiwa katika nafasi za watendaji waandamizi, ningependa kuongezea na kuwajulisha kwamba, Naibu Katibu Mkuu, Migiro na Vijar Nambiar wamewasilisha kwangu maombi yao ya kutaka kuachia nafasi zao, ili kuniruhusu kuunda timu mpya ya maofisa waandamizi nitakaofanya nao kazi katika awamu ya pili ya uongozi wangu,” alisema Ban Ki Moon.

Katibu Mkuu huyo alimpongeza Migiro kwa ushirikiano mkubwa na usio na shaka wala doa aliompa katika kipindi chote cha miaka mitano iliyopita akiwa msaidizi wake wa karibu.

“Amenipatia ushirikiano mzuri sana, alinishauri kwa busara na amejituma sana na kwa kuadilifu mkubwa katika kukabiliana na changamoto nyingi zilizoikabili taasisi hii wakati wa awamu yangu ya kwanza ya uongozi,” alisisitiza Ban Ki Moon.

Hata hivyo alisema Migiro ataendelea kuwapo ofisini hadi Juni mwaka huu ili kuratibu na kusimamia kipindi cha mpito pamoja na maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo Endelevu (RIO+20).

Pamoja na Migiro kuwasilisha ombi lake, wapo pia baadhi ya watendaji waandamizi ambao nao wameonyesha nia ya kuachia nafasi zao ili kupisha menejimenti mpya.

Watendaji wengine watakaoondoka na ambao wengi wao walikuwa katika awamu ya kwanza ya uongozi wa Ban ki Moon ni kutoka Idara za Utawala, Maendeleo, Huduma za Mikutano, Habari, Ofisi ya Upokonyaji wa silaha na Mshauri wa Masuala ya Afrika.

Wengine ni wasimamizi wa Idara za Uchumi za Afrika na Ulaya, waratibu wa mifuko ya maendeleo na Idadi ya watu UNDP na UNFPA.

Aidha, wamo pia wawakilishi maalumu wa katibu mkuu wanaohusika na masuala ya watoto katika migogoro ya kivita, na uzuiaji wa mauaji ya kimbali, ambao wanatarajiwa kuachia nafasi zao katikati ya mwaka huu.

Mchakato wa kujaza nafasi nane zitakazoachwa wazi katika ngazi za ukatibu mkuu msaidizi (Under-Secretary General) umekwisha anza na ujazaji wa nafasi hizo ambao utakuwa wa uwazi utazingatia sana sifa na uwezo wa mtu, uwiano wa kikanda na jinsia.

Thomas Lubanga apatikana na hatia









Mahakama ya kimataifa ya jinai ICC iliyoko the Hague, imempata na hatia ya uhalifu wa kivita mbabe wa zamani wa kivita katika Jamuhuri Ya Kidemokrasia ya Congo Thomas Lubanga.
Hukumu hiyo ndiyo ya kwanza kutolewa na mahakama ya ICC tangu kubuniwa kwake zaidi ya muongo mmoja uliopita. Hata hivyo mahakama itaamua baadaye hii leo adhabu atakayopata Lubanga.
Lubanga alipatikana na hatia ya kuwasajili watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na mitano kama wanajeshi wake wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kaskazini mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya congo.
Lubanga pia alisemekana kuwa kiongozi wa kundi la waasi wakati wa makabiliano ya kikabila katika eneo lenya utajiri wa dhahabu nchini humo.
Upande wa mashtaka ulimtuhumu Lubanga kwa kutumia watoto kama watumwa wa ngono, walinzi wake na wapiganaji wake.
Katika uamuzi uliopitishwa kwa kauli moja, majaji watatu waliokuwa wanasikiliza kesi dhidi ya Lubanga, walisema kuwa ushahidi dhidi ya Lubanga ulithibitisha kuwa kundi la waasi lilioongozwa na Lubanga pia linapaswa kuwajibishwa kwa makosa ya kusajili watoto kama wapiganaji waliopigana kwenye msityari wa mbele.
Lubanga, aliyekamatwa mwaka 2005, huenda akahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi kupitisha hukumu ya kunyongwa.

Wednesday, March 14, 2012

MALI ALIZOIBIWA WAZIRI MALIMA ZAKUTWA KWA 'MA-MDOGO'





KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo amesema kuwa aliyemwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni katika hoteli ya Nashera mkoani Morogoro sio mwanamke.

Kamanda huyo alisema mtuhumiwa aliyekamatwa na polisi alipohojiwa alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi nyumbani kwa mama yake mdogo na kwamba waziri Malima hakuwa na bunduki aina ya SMG, kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Naibu Waziri Malima alikumbwa na mkasa huo uliozua maswali mengi saa 10 alfajiri ya kuamkia Machi 9, mwaka huu baada ya watu kueleza sababu tofauti za wizi huo.Baadhi ya watu walidai kuwa Waziri huyo alikuwa na mtu chumbani anayesaidikiwa alitoroka na vitu hivyo na wengine walidai kuwa aliibiwa na mtu aliyepitia dirishani baada ya kufungua dirisha.

Chialo aliliambia Mwananchi jana kuwa mmoja wa watuhuniwa wa tukio hilo alipobanwa alieleza wazi kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo.“Unajua haya mambo yanakuzwa lakini hayana ukweli wowote, yupo mtu mmoja ambaye baada ya kumbana alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo,” alisema Chialo.

Akizungumzia taarifa kuwa Waziri Malima alikuwa na SMG katika chumba chake alisema “Hakuwa na SMG alikuwa na bastola, SMG ni silaha ambayo hata mimi Kamanda wa polisi siwezi kutembea nayo”Alifafanua kuwa silaha hiyo ya kivita humilikiwa kwa kibali maalumu na kwamba si rahisi kwa mtu kuwa nayo kienyeji.

“Hata silaha ambazo alikuwa nazo Waziri Malima ni za kawaida na anazimiliki kihalali” alisema Chialo.

Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo, Machi 9 mwaka huu Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Hamisi Seleman alisema ingawa uchunguzi unaendelea kufanyika, taarifa za awali zilieleza kuwa mtu asiyejulikana alivunja dirisha la chumba namba 125 alichopanga Naibu Waziri huyo kisha kuingia ndani na kuiba vitu hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni.

"Vitu alivyoibiwa ni pamoja na laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani ya Sh5.6 milioni.

Vinasa sauti viwili vya digitali na headphone zake zote ambavyo thamani yake ni Sh 1 milioni na simu tatu aina ya Nokia C6 ya Sh500,000, Nokia E200 ya Sh250,000 na Blackberry zenye thamani ya Sh5.5 milioni," alisema kamanda huyo na kuongeza:

"Vitu vingine ni pete mbili za almasi zenye thamani ya Sh2.5 milioni, Dola 4,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh6.5milioni, Sh1.5 milioni, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo, baraghashia mbili zenye thamani ya Sh50,000 na nyaraka mbalimbali za Serikali.

"Kaimu kamanda huyo alisema kuwa polisi waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa mtu aliyeiba vitu hivyo hakuwa amevaa viatu kutokana na nyayo za miguu yake zilizoonekana nje ya chumba alichokuwa naibu waziri huyo.Kaimu kamanda huyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro, alisema kuwa hata hivyo, mwizi aliyeiba vitu hivyo hakuiba bastola na bunduki aina ya SMG alizokuwa nazo Naibu Waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu iliyowazi.

Katika hatua nyingine, polisi mkoani Morogoro, wanawashikilia watu watano wanaotuhumiwa kumwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Malima katika Hoteli ya Nashera wiki iliyopita huku asilimia 90 ya vitu vilivyoibiwa vikipatikana kutoka kwa watuhumiwa hao.

Kamanda Chialo alisema waliokamatwa kuwa mmoja ni mkazi wa Chamwino kwa Mgulasi na wengine ni wakazi wa Mafiga Manispaa ya Morogoro ambao kwa pamoja wanadaiwa kushiriki katika tukio hilo la wizi.

Sunday, March 11, 2012

MASHINE YA KUINUA MATITI YA WANAWAKE YAINGIA NCHINI TANZANIA








Na Julieth Kulangwa, Gazeti la Mwananchi.


*WANAWAKE WAFURIKA KUPATA HUDUMA

BIASHARA huria imezua mengi. Hali kadhalika Sayansi na Tekenolojia nayo, imeleta mengi. Katika kuwaondolea kero wanawake wenye matiti yaliyosinyaa hapa nchini, wataalamu kutoka China wameanza kutoa huduma ya kunyanyua matiti hayo kwa kutumia mashine maalumu.

Wachina wamejipatia umaarufu katika kuleta bidhaa mbalimbali hapa nchini, zikiwamo za kuongeza nguvu za kiume, kupunguza uzito, kuotesha nywele, kujichubua (kumfanya mtu mweusi awe mweupe), kuongeza makalio nk.

Huduma hiyo ya kusimamisha matiti yaliyolala, imeanza kutolewa katika Saluni ya Blue Palace, iliyopo nyuma ya Shule ya Mapambano, Sinza jijini Dar es Salaam.

Haikuwa rahisi kuweza kuamini kuwa vitu kama hivi vinaweza kupatikana Tanzania. Mwananchi Jumapili lilifunga safari mpaka kwenye saluni hiyo inayomilikiwa na Sarafina Mtweve, kujionea jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi.


Mbali na meneja wa saluni hiyo, Trust Mwembe, pia alikuwepo mtaalamu kutoka China aitwaye, Ciisy Pang, ni binti wa miaka 23 tu, lakini anasema kwa miaka minne amefanya kazi hiyo na kuwasaidia wanawake mbalimbali waliokuwa wakikerwa na matiti yaliyolegea au kuanguka.

Pang na kundi lake wanatoa huduma hii kwa gharama ya Sh150,000 kwa kuanzia, ingawa wanahisi gharama hizo zitapanda katika siku chache zijazo.

Jinsi matiti yanavyosimamishwa

Mashine hiyo inayoitwa ‘Beauty Machine’ ina uwezo wa kusimamisha matiti ya kila saizi kwa kuwa huambatanishwa na vibakuli (cups) kama unavyoona pichani.

Kazi kubwa ya mashine hiyo ni kuamsha misuli ambayo hushikilia nyama za matiti.


Pang anasema, zoezi la kusimamisha matiti huchukua wiki tatu mpaka sita, inategemea aina ya mteja na wakati mwingine juhudi zake.

Mtaalamu huyo ambaye anazungumza Kichina na kutafsiriwa na meneja wa saluni hiyo, anaelezea namna anavyofanya kazi ya kuyarudisha matiti kwa muda huo.

“Kwanza unapaswa ujue kuwa hatutumii dawa yoyote katika zoezi hili, mteja wetu akifika hapa, kinachotumika ni mashine tu ambayo hutumia umeme kama zilivyo dryer za nywele,“Baada ya kumlaza katika kitanda kile, tunachukua kitu mfano wa bakuli (cups) mbili kulingana na ukubwa wa matiti yake, tunayatumbukiza humo, kisha tunawasha mashine,” anasema Pang.

Mtaalamu huyo anasema mashine hiyo ikiwashwa inavuta kama ‘vacuum’, na inaweza kuongezwa kasi au kupunguzwa kama inavyofanyika kwenye mashine za kufanyia mazoezi.

“Tunaiwasha mashine kwa muda wa dakika 45, mteja atachagua siku mbili katika wiki za kufanya zoezi hili mpaka litakapokamilika,”anasema Pang.

Tangu mashine hiyo iwasili nchini, takribani mwezi mmoja uliopita, Pang anasema ana wateja wanane anaowahudumia kwa nyakati tofauti ambao wamekiri kuwa maendeleo yanatia moyo.

Ni kweli mashine hii inasaidia?

Akizungumza kwa njia ya simu, mmoja wa wateja anayepata huduma hiyo ambaye alijitambulisha kwa jina moja tu Irene anasema, ni wiki ya tatu sasa tangu aanze kupata huduma hiyo, anakiri kuwa matiti yake sasa yameanza kuwa magumu tofauti na mwanzo.

“Kusema kweli nilikuwa na matiti yaliyosinyaa wala si kulala tu kama ulivyouliza, ila naona sasa yameanza kuwa magumu na kurudi juu kidogo,” anasema Irene.

Akizungumzia ugumu anaoupata katika zoezi hilo, anasema safari za kila wiki saluni na zile dakika 45 za kukaa kwenye mashine zinamchosha, lakini kwa kuwa amedhamiria, amejitoa mpaka zoezi hilo litakapokamilika.

Matiti yanaweza kulegea tena?

Pang anasema kama matiti yanalegea kwa sababu fulani mfano uzazi wa watoto wengi, basi yanaweza kulegea tena kama mtu atajifungua na kunyonyesha kwa muda huo.Aidha anasema wanawake wenye matiti makubwa, ni rahisi kuanguka kama hawatayavalisha sidiria kwa muda mrefu.

“Wanawake wenye matiti makubwa huwa nawashauri kuvaa sidiria hasa wakati wa mchana na usiku wanaweza kuacha kuzivaa, hii inasaidia kuimarisha misuli inayoyabeba matiti,” anasema Pang.

Jamii inazungumziaje jambo hili

Baada ya kusikia kuwepo kwa mashine hii nchini, wanawake mbalimbali wamesema wanatamani kupata huduma hiyo lakini wengine, walionyesha woga juu ya matokeo yake.

“Ni kweli baada ya kunyonyesha watoto wawili sasa matiti yamelegea kabisa, natamani yarudi kama wakati ule wa usichana wangu, lakini nahofia huenda mbele ya safari nikapata madhara,” anasema Linda Masatu.

Linda anaongeza kusema kuwa ni vizuri mwanamke akawa na matiti yaliyojaa vizuri, lakini anahofia njia zinaweza kuwa na madhara, huku akisema kama ingetokea njia nyingine ya asili asingesita kuifuata.

Naye Batuli Famau, anasema mwanamke anapokuwa na matiti yaliyosinyaa mvuto wake hupungua, hata anapovaa sidiria anakuwa amebadili mwonekano wa nje tu, lakini ndani bado anakuwa vilevile.

“Mwanamke mrembo ni yule mwenye matiti mazuri, sasa inapobidi kutumia njia fulani ili yarudi kama tulipokuwa vigoli, tutafanya tu ili mradi kama njia hizo hazitatuangamiza,” anasema

Wanaume nao wameonekana kuunga mkono zoezi la kusimamisha matiti ingawa wengine hawaungi mkono utumiaji wa mashine hii.Augustino Magara anasema: “Ni kweli mwanamke mwenye matiti magumu anavutia kuliko yaliolegea na kulala, lakini sasa tuwe makini kabla wake zetu hawajaumia katika mashine, hizi”

“Wote tunajua sababu zilizosababisha matiti ya wake zetu yalegee, sioni sababu ya kusema tunataka yaliyomagumu, tuwapende wake zetu hivi hivi na tuwape moyo,” anasema Nganara.

Dk Innocent Mosha wa Kitengo cha Patholojia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, anasema ni vigumu kwa wataalamu wa afya kugundua madhara ya mashine hizo kwa haraka hadi pale uchunguzi utakapofanyika.

“Ingelikuwa mazoezi hayo yanachukua muda mfupi, kweli tungepata wasiwasi kwa kuwa, unapoisimamisha misuli kwa haraka ni lazima madhara yatokee, lakini hili la mazoezi, bado sifahamu,” anasema Dk Mosha.

MECHI YA YANGA,AZAM YAINGIZA SH.MIL. 72

MECHI YA YANGA,AZAM YAINGIZA SH.MIL. 72















AZAM, YANGA ZAINGIZA MIL 72/-
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Azam lililochezwa Machi 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 72,731,000.

Jumla ya watazamaji 19,339 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000 viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati kwa VIP A ilikuwa sh. 15,000.

Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 11,303,932.20 kila timu ilipata sh. 14,726,592.20, uwanja sh. 4,908,864.07.

Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,963,545.63, TFF sh. 4,908,864.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,454,432.03, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 490,886.41 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 4,908,864.07.

Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. waamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna sh. 40,000, tiketi sh. 3,540,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.

Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata tena sh. 1,353,730 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata tena sh. 1,160,340.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)






MAMBO YA SWIMMING HAYO











You might also like:

MECHI YA YANGA,AZAM YAINGIZA SH.MIL. 72







AZAM, YANGA ZAINGIZA MIL 72/-
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Azam lililochezwa Machi 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 72,731,000.

Jumla ya watazamaji 19,339 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000 viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati kwa VIP A ilikuwa sh. 15,000.

Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 11,303,932.20 kila timu ilipata sh. 14,726,592.20, uwanja sh. 4,908,864.07.

Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,963,545.63, TFF sh. 4,908,864.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,454,432.03, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 490,886.41 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 4,908,864.07.

Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. waamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna sh. 40,000, tiketi sh. 3,540,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.

Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata tena sh. 1,353,730 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata tena sh. 1,160,340.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Saturday, March 10, 2012

KINGKIKI AKONGA NYAYO ZA WAPENZI WAKE KWA KITAMBAA CHEUPE,ONYESHO LILIDHAMINIWA NA KINYWAJI CHA DODOMA WINE!!

jana ilikuwa mambo swaaaafiiii kitambaa cheupe

MKALI WA FACEBOOK KUPIGA SHOO LEO VIWANJA VYA POSTA KIJITONYAM​A KUANZIA SAA MOJA JIONI!!





Msanii wa Mziki kutoka South Africa, Cleopas Monyepao (DJ Cloe) kulia akizungumza na waandishi wa habari, Dar es salaam jana kuhusu onesho lake la leo litakalofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama kushoto ni Msanii aliyeongozana nae Dumiseni Mkihanya.(Picha na www.burudan.blogspot.com)

Msanii wa Mziki wa kizazi kipya nchini, Omary Nyembo A.K.A Ommy Dimpoz kushoto akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam leo kuhusu Onesho lake litakalofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama kulia ni msanii kutoka, South Africa, Cleopas Monyepao (DJ Cloe) na Dumiseni Mkihanya na Meneja wa Kinywaji cha Savana, Diana Musheruzi.(Picha na www.burudan.blogspot.com)


Na Mwandishi Wetu

CLEOPAS Monyepao maarufu kama DJ Cleo mkali wa nyimbo ya Facebook kutoka Afrika Kusini kesho anatarajia kutoa burudani katika viwanja vya Posta, Kijitintama Dar es Salaam.

Dj Cleo ameambatana na wachezaji wake Dumisani Makihanya 'Bleksem' na Dj Soul T ambaye amekuwa akionekana katika video mbalimbali za nyimbo zake.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Dj Cleo alisema amefurahishwa sana na ujio wake hapa nchini ikiwa ni kwa mara ya kwanza na hiyo ni kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi mbili.

Alisema, anaamini katika onesho lake hilo la kesho atajifunza mengi kutoka kwa Watanzania ikiwa ni pamoja na kuwajua wanamuziki na muziki wa hapa nchini sambamba na Utamaduni kwa kiasi fulani.

Aliongeza kuwa anahitaji sana kujifunza utamaduni wa Tanzania kwani nchi hizo zinashirikiano mkubwa na zinaendana kwa mambo mbalimbali kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na muonekano wa wananchi wake.

Alisema, kwa upande wa burudani atawapa mashabiki burudani nzuri na ambayo wataridhika nayo ingawa mashabiki wengi wanaujua wimbo wake wa Facebook lakini yeye ananyimbo nyingi hivyo zitakuwa ni 'Supries' kwao.

"Watu wengi wanaujua wimbo wangu wa Facebook lakini zipo nyimbo nyingi ambazo zitakuwa ni mpya kwao na ninaamini watazipenda hivyo waje kwa wingi ili waweze kujionea na kusikia," alisema.

Naye kwa upande wake mmoja wa wanamuziki ambao wataimba jukwaa moja na DJ Cleo, Omari Nyembo 'Ommy Dimpoz' alisema, anajisikia faraja kubwa kupanda jukwaa moja na msanii huyo kwani anaimani naye atajifunza mengi kutoka kwa msanii.

Alisema, kupanda jukwaa moja na wasanii wa nje kunawasaidia muziki wao kufahamika Kimataifa zaidi kwani utajulikana ukilinganisha kazi yake hasa mwanamuziki huyo ni ya Udj.

Sambamba na wanamuziki hao pia jukwaa hilo litapambwa na Suma lee, Dully Sykes, Juma Nature, Tip Top Conection, Wanaume Halisi, Chege na Temba, Wanaume TMK na Wakali Dancers

Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938

- +255713406938

Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

KIKWETE AKUTANA NA MADAKTARI IKULU












Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwakaribisha ikulu jijini Dar es salaam viongozi wa Chama cha madaktari nchini. Wa pili kushoto ni Mratibu wa mgomo wa madaktari, Stephen Ulimboka na Kulia ni Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwakatika mazungumzo na viongozi wa Chama Cha Madaktari nchini(MAT) ikulu jijini Dar esSalaam leo mchana(picha na Freddy Maro)

Friday, March 9, 2012

Konyagi wawanoa waliojiunga nayo!!Vituko vyatawala ktk kupiga picha ya pamoja!!

Mmoja anaficha uso


Mkufunzi akitoa maelezo yake

kamsukuma

Mmoja kashika kichwa na mwingine uso

Angalizoo kwa umma

Ni heri hekima inayokuja kwa kuchelewa kuliko inayokosekana kabisa. Maana, ni heri kutibiwa na daktari aliye kazini na moyo mkunjufu kuliko kutibiwa na daktari liyelazimishwa kwa nguvu kurudi kazini huku akiwa na kinyongo. Wahenga walinena; unaweza umlazimisha punda kwenda mtoni, lakini kamwe huwezi kumlazimisha kuyanywa maji. Hilo la mwisho ni a hiyari, kama ilivyo kwa tabasamu, kwamba unaweza kumlazimisha mwanadamu kupiga makofi, lakini kamwe huwezi kumlazimisha kutabasamu, hilo la mwisho...

MAHAKAMA KUU YASITISHA MGOMO WA MADAKTARI NCHINI








Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, leo (Alhamisi Machi 8, 2012) imetoa uamuzi wa kusitishwa mara moja kwa mgomo wa Madaktari ulioitishwa nchi nzima tangu jana (Jumatano Machi 7, 2012).




Katika amri yake ya pili, Mahakama Kuu pia imekitaka Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari kuwatangazia wanachama wao mara moja kupitia Vyombo vya Habari kusitishwa kwa mgomo huo nchi nzima kama walivyowatangazia wakati wanauitisha mgomo wenyewe.




Mahakama Kuu pia imeamuru pande zote mbili, yaani Serikali kwa upande mmoja na Chama cha Madaktari na Jumuiya ya Madaktari, kwa upande mwingine, kutumia fursa zilizopo katika kutatua mgogoro wa kikazi uliopo kati yao kwa haraka.




Uamuzi huo wa Mahakama Kuu imetolewa na Jaji R.M. Rweyemamu, baada ya kusikiliza ombi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari na Jumuiya ya Madaktari kuitaka itoe zuio kwa mgomo huo.




Akitoa uamuzi huo, Jaji Rweyemamu alisema anazingatia madhara ambayo mgomo huo ungeleta kwa jamii kwa vile huduma za tiba ambazo madaktari walitaka kugoma kuzitoa ni miongoni mwa huduma muhimu zilizotajwa kwenye Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Namba 6 ya Mwaka 2004.




Uamuzi huo, ni kama ifuatavyo:




Leo, tarehe 8, Machi 2012, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, mbele ya Jaji R.M. Rweyemamu, baada ya kusikiliza Ombi No. 24 la 2012 lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Mwombaji) dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari (Walalamikiwa), imetoa uamuzi ufuatao:




i) Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari pamoja na Wanachama wao, kusitisha Mgomo waliouanzisha rasmi tarehe 7 Machi 2012 nchi nzima na kurejea kazini mara moja kwa kuendelea na kazi zao kama kawaida, mara tu Amri hii itakapowafikia. Aidha, waombaji watatakiwa kutoa Kiapo cha kuthibitisha kwamba wamewasilisha Amri hiyo kwa Walalamikiwa na kuwasilisha Kiapo hicho Mahakama Kuu – Divisheni ya Kazi kesho tarehe 9, Mach 2012.




ii) Mara baada ya Amri hii kuwasilishwa kwa Walalamikiwa (Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari) watatakiwa kuwatangazia Wanachama wao kupitia Vyombo vya Habari kusitishwa kwa Mgomo huo Nchi nzima kama walivyowatangazia wakati wa kuitisha Mgomo huo;




iii) Mahakama inaamuru pande zote mbili (Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania pamoja na Jumuiya ya Madaktari) kutumia fursa za Kisheria zilizopo katika kutatua Mgogoro wa Kikazi uliopo kati yao kwa haraka.




Imetolewa na:




Ofisi ya Waziri Mkuu,


S.L.P. 3021


DAR ES SALAAM.


Alhamisi Machi 8, 2012

SIMBA YAPANGA KUGOMEA MECHI ZA UWANJA WA TAIFA





KLABU ya soka ya Simba imetishia kugomea kucheza mechi zake katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, pia kuzuia wanachama wake kuingia uwanjani, kutokana na uonevu wanaofanyiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika mchakato mzima wa mapato ya mlangoni.


Hatua hiyo inafuatia juzi TFF kuikata Simba mgao wake wote wa shilingi mil.3.5 ilioupata kupitia mapato ya mchezo wao wa ligi kuu baina yao na Kagera Sugar ya Kagera kwa madai ya fidia ya shilingi mil.tano wanazotakiwa kulipa baada ya wanaodaiwa mashabiki wa Simba kuharibu viti vya uwanja huo katika mechi baina ya Simba na Kiyovu iliyofanyika jumapili iliyopita.


Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage amesema leo kwamba wanashangazwa na uonevu wa wazi unaofanywa na TFF , kwa kuwa uwanja huo si mali yao na wamekuwa wakilipa fedha nyingi kabla ya mchezo kama tahadhari kwa uharibifu wowote utakaotokea lakini haijulikani fedha hizo zinakwenda wapi.

“Mfano mechi yetu na Kagera Sugar juzi mapato yalikuwa mil.24 na baada ya makato ya mamlaka mbalimbali zilibaki mil.7 na vilabu kugawana hivyo kila timu kupata mil.3.5, huu ni unyonyaji kabisa kwani pamoja na vilabu kugharamika kwa fedha nyingi kwenye maandalizi lakini mwisho wa siku wanakuja kufaidika watu wasiochangia mapato yoyote,”Alisema Kwa habari zaidi tembelea :http://mamapipiro.blogspot.com/

Hatimaye:-


SERIKALI YATANGAZA RASMI MIKOA MIPYA MINNE NA WILAYA 19









Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
SERIKALI imetoa matangazo rasmi ya Serikali (Government Notices) kuhusu uanzishaji wa mikoa mipya minne na wilaya mpya 19 ambayo yamechapishwa tangu Machi 2, mwaka huu.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema matangazo hayo ambayo yalisainiwa na Rais Jakaya Kikwete tangu Machi mosi, 2012, yanabainisha mikoa mipya kuwa ni Geita, Katavi, Njombe na Simiyu. Mikoa hii imechapishwa katika Tangazo la Serikali Na. 72.

Wilaya 19 ambazo zimeanzishwa na kuchapishwa katika Tangazo la Serikali Na.73 ni Buhigwe, Busega, Butiama, Chemba, Gairo, Ikungi na Itilima. Wilaya nyingine ni Kakonko, Kalambo, Kaliua, Kyerwa, Mbogwe, Mkalama na Mlele. Nyingine ni Momba, Nyang’hwale, Nyasa, Uvinza na Wanging’ombe.

Kwa mujibu wa matangazo hayo makao makuu ya mikoa hiyo mipya minne yatakuwa kama ifuatavyo: Geita (Geita), Simiyu (Bariadi) Njombe (Njombe) na Katavi (Mpanda).

Mikoa hiyo itakuwa na wilaya zifuatazo; Geita utakuwa na wilaya tano za Bukombe, Chato, Geita, Mbongwe na Nyang’hwale. Mkoa wa Katavi utakuwa na wilaya mbili za Mlele na Mpanda. Mkoa waNjombe utakuwa na wilaya nne za Makete, Njombe, Ludewa na Wanging’ombe wakati mkoa wa Simiyuutakuwa na wilaya tano za Bariadi, Busega, Maswa, Meatu na Itilima.

Makao makuu ya wilaya mpya zilizoanzishwa ni kama ifuatavyo: Buhigwe (Buhigwe); Busega (Nyashimo); Butiama (Butiama); Chemba (Chemba); Gairo (Gairo); Ikungi (Ikungi) Itilima (Lagangabilili); Kakonko (Kakonko); Kalambo (Matai) na Kaliua (Kaliua).

Nyingine ni Kyerwa (Rubwera); Mbogwe (Mbogwe); Mkalama (Nduguti); Mlele (Inyonga); Momba (Chitete); Nyang’hwale (Kharumwa); Nyasa (Mbamba Bay); Uvinza (Lugufu) na Igwachanya (Wanging’ombe).

Julai 2010, kabla Rais Kikwete hajatoa hotuba ya kulivunja Bunge, Serikali ilitoa uamuzi wa kuunda mikoa mipya minne na wilaya mpya 21. Hata hivyo, baada ya kuhakiki mipaka ya maeneo hayo yote na kuandaa maelezo ya mipaka hiyo vizuri (boundary descriptions), wilaya zilipunguzwa na kubakia 19.


IMETOLEWA NA:


OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 3021,

DAR ES SALAAM.

ALHAMISI, MACHI 8, 2012.

Irene K. Bwire,


Email: irenekaki@yahoo.com

"We cannot build our own future without helping others to build theirs"

- Bill Clinton, American 42nd President