header

nmb

nmb

Friday, July 29, 2016

MAZOEZI MAKALI YANAENDELEA KATIKA KAMBI YA SUPER D COACH UHURU GYM KARIAKOO


Mabondia Faraji Sayuni kushoto na Hassani Kiwale wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika kambi ya Super D Coach Uhuru GYM Kariakoo mabondia wote hawo watapanda uringoni agost 8 katika ukumbi wa kobelo pub manzese Dar Es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS

 Bondia Hassani Kiwale kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Faraji Sayuni wakati wa mazoezi yao yaliyofanyika katika kambi ya Super DCoach Uhuru GYM Kariakoo Dar es salaam mabonda hawo watapanda uringoni Agost 8 kuwakabili wapinzani wao katika ukumbi wa kobelo pub manzese Dar Es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Hassani Kiwale kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Faraji Sayuni wakati wa mazoezi yao yaliyofanyika katika kambi ya Super DCoach Uhuru GYM Kariakoo Dar es salaam mabonda hawo watapanda uringoni Agost 8 kuwakabili wapinzani wao katika ukumbi wa kobelo pub manzese Dar Es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwasimamia mazoezi mabondia Faraji Sayuni kushoto na Hassani Kiwale wakati ya mazoezi yao yanayoendelea katika kambi ya Super D coach Uhuru GYM Kariakoo Dar Es Salaam 


Na Mwandishi Wetu
MPAMBANO wa ubingwa wa taifa wa kg 57 utagombaniwa na mabondia Kais Rashidi Na Faraji Sayuni siku ya Agost 8 katika ukumbi wa Kobelo Pub Manzese Dar Es Salaam  

mpambano uho wa raundi kumi za ubingwa umeratibiwa na Promot Miraji Uliza ambapo kutakuwa na mapambano mengine mbalimbali ya mchezo wa masumbwi nchini

mabondia wengine watakaopanda siku hiyo ni Abdallah Pazi atakaezipiga na Said Mkone wakati godrack Mrema atakumbana na Hassani Kiwale wakati Omari Uliza atazipiga na Bruno Fadhili na Said Jelemi atamkabili Azizi Kondo na Saleh Mkalekwa atacheza na Salum Ngula na Azizi Uliza atacheza na Mohamed Matimbwa

pamoja na mapambano mengine mengi

Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha  'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.


Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

No comments:

Post a Comment