Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete ameshtushwa na kufadhaishwa na taarifa za kifo cha Mjumbe
waTume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Sengondo Mvungi kilichotokea jana,
Jumanne, Novemba 12, 2013 kwenye Hospitali ya Milpark, Johannesburg,
AfrikaKusini.
Katika salamu za rambirambi ambazo amemtumia Mwenyekitiwa Tume hiyo,
Jaji Joseph SindeWarioba, Rais Kikwete amesema kuwa amepokea kwa mshtuko
mkubwa na fadhaha taarifa za kifo cha Dkt. Mvungi. “Kwa hakika ni
taarifa iliyonisumbua na kunipa huzuni nyingi.”
Rais Kikwete amesema kuwa hakuna shaka kuwa katika maisha yakeDkt.
Mvungi ametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Tanzania kwa namna
mbalimbali na kuwa kifo kimemfika wakati Taifa la Tanzania lilikuwa bado
linahitaji busara, hekima na mchango wake katika mchakato mzima wa
kusaka Katiba mpya.
“Kuanzia alipokuwa mwandishi wa habari katika Magazeti ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) ya Uhuru na Mzalendo, hadi uhadhiri wake katika Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, hadi uwakili katika Kampuni ya South Law
Chambers, hadi uongozi wake katika Chama cha NCCR-Mageuzi, hadi uamuzi
wake wa kugombea Urais wa Tanzania mwaka 2005 na sasa akiwa Mjumbe wa
Tume ya Katiba, Dkt. Mvungi ametoa mchango wake mkubwa sana katika
maendeleo ya nchi yetu. Na hili hatutalisahau,” amesemaRaisKikwete.
“Kwa masikitiko makubwa, nakutumia wewe Jaji Joseph Warioba,
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba salamu za rambirambi za dhati
ya moyo wangu nikiombeleza kifo cha Dkt. Mvungi. Nakupa pole nyingi
wewe Mwenyekiti, wajumbe wa Tume na wafanyakazi wote wa Tume kwa
kuondokewa na mwenzenu. Naungana nanyi kuombleza msibahuo mkubwa.”
“Aidha, kupitia kwako, natuma pole nyingi kwa wana-familia, ndugu,
marafiki nan majirani wa Dkt. Mvungi kwa kuondokewa na mhimili,msimamizi
wafamilia na ndugu. Wajulishe kuwa niko nao katika msiba huu
mkubwa.Wajulishe kuwa msiba wao ni msiba wangu pia. Muhimu waelewe kuwa
binafsi naelewa machungu yao katika kipindi hiki kigumu na namwomba
Mwenyezi Mungu awape subira waweze kuvuka kipindi hiki kigumu kwa sababu
yote ni mapenzi yake.”
Amemalizia Rais Kikwete: “Napenda kuungana nao katika kumwomba
MwenyeziMungu, Mwingi wa Rehema, aiweke mahali pema roho ya Marehemu
Dkt. Sengondo Mvungi. Amina.”
No comments:
Post a Comment