header

nmb

nmb

Friday, November 15, 2013

VIONGOZI WAPATANISHI WA PALESTINA WAJIUZULU

VIONGOZI WAPATANISHI WA PALESTINA WAJIUZULU

Viongozi waliowasilisha barua za kujiuzulu ni pamoja na mpatanishi mkuu Saeb Erakat na Mohammed Shtayyeh, hatua walioichukua baada ya Waziri wa Makaazi na Ujenzi wa Israel, Uri Ariel kutangaza kuendeleza ujenzi wa nyumba zipatazo 24,000 kwenye Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki.
Hata hivyo mpango huo mpya ulikosolewa na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na alimuamuru Waziri Ariel kuusitisha akisema kuwa utasababisha mvutano usio wa lazima na jumuiya ya kimataifa.Afisa wa chama cha ukombozi wa Wapalestina-PLO, Xavier Abu Eid amesema Erakat na Shtayyeh waliwasilisha barua zao kwa Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, kabla ya Netanyahu hajasitisha ujenzi huo. Netanyahu amesema waziri wake alifanya maamuzi hayo peke yake bila kumshirikisha. Jana Jumatano (13.11.2013) Abbas alizungumza kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry anayesimamia mazungumzo hayo kwa kiasi kikubwa, na akamuhakikishia nia yake ya kutaka kuendelea kwa mazungumzo hayo. Abbas amesema mazungumzo yataendelea hata kama ujumbe wa wapatanishi wa Palestina umejiondoa.
Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Misri cha CBC, Abbas amesema wanajaribu kuwashawishi wapatanishi hao kurejea kwenye mazungumzo hayo ya amani, ama watachagua wapatanishi wapya. Hata hivyo, bado haijafahamika wazi iwapo Abbas atakubali barua hizo za kujiuzulu, hadi hapo atakapokubali kusaini.Afisa mwandamizi wa PLO, Hanan Ashrawi amesema iwapo hatua ya kujiuzulu wapatanishi hao itakuwa rasmi, itakuwa vigumu kwa Abbas kutafuta wapatanishi wengine, kwa sababu hakuna mtu ambaye anataka kujihusisha katika mchakato wa amani ambao mwelekeo wake haueleweki.

No comments:

Post a Comment