Mabondia
Issa Omar na Shaban Madilu ambao wanacheza pambano lao la raundi kumi ubingwa wa UBO international, wakisindikizwa
na wakongwe wa masumbwi nchini Joseph Marwa atakaezipiga na amour mzungu katika
pambano la kisasi ,baada ya mzungu kupigwa na marwa miaka saba iliyopita
jumapili hii ndani ya ccm mwinjuma anataka ajiulize ilikuwaje na amepata uzoefu
wa kutosha wa kulipa kisasi.
Mabondia
wote hao pamoja na uzito wa juu Ramadhan kido na musa mbabe wanategemea kupima
afya zao na uzito siku ya jumamosi saa nne asubui hapohapo ukumbini CCM
Mwinjuma – mwananyamala zoezi zima la upimaji litaongozwa na dr donard Madono
akisaidiwa na Emanuel mlundwa.
Mpambano huo
ulioandaliwa na bigright promotion na
kusimamiwa na PST kama mwakilishi wa UBO nchini unategemea kuwakutanisha
mabondia mbalimbali wenye uwezo mzuri na kuwavutia washabiki wa mchezo huo kwa
kushuhudia mapambano zaidi ya tisa kwa wakati mmoja na mabondia wanaotegemea
kupima siku ya jumamosi ni Ide mnali toka mtwara atakaezipiga na zumba kukwe wa
dare s salaam, Husein Mbonde atazipiga na mwaite juma,Martin Richard atapigana
na Faraji Sayuni, Salum Chandonga atazipiga na mdogo wake amour mzungu ,Mohamed
mzungu. Herman Richard na kade hamis, kani west na Nasor Hatibu,james Edmond na
julias anastaz .pia kutakuwa na maonesho ya ngumi za watoto wenye vipaji.
Mpaka leo
hii haijaripotiwa kama kuna tatizo lolote na mabondia karibu wote wapo katika hali nzuri na wapo
tayari kwa mpambano
No comments:
Post a Comment