Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan
akifafanua Jambo wakati alipotembelea Mradimpunga wa Umwagiliaji kwenye
Bonde la Mpunga la Jendele kulia Mwenyekiti wa Tasaf Jendele Ali
Mussa waziri alifanya Ziara ya Wilaya ya Kati Unguja
kukutembelea Mradi Uliofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania
Na Ali Issa Maelezo Zanzibar 4/4/2013
Waziri wa nnchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
Samia Suluhu Hassan amesema kuna umuhimu
mkubwa kwa wana nchi kuituza na kuindeleza miradi inayo fadhiliwa na Serikali
zotembili na washirika wa maendeleo ili
miradi hiyo indelee kuwanufaisha wananchi na kutimia lengo lililo kusudiwa.
Hayo ameyasema leo huko Jendele wilaya ya
kati Mkoa wa Kusini Unguja wakati alipo fanya ziara kutembelea miradi mbali mbali ya kilimo ilio
fadhiliwa na TASAF kupitia Serikali ya muungano Tanzania.
Mratibu wa wa Programu ya kuimarisha huduma za kilimo Bw Zaki Khamis
Juma akimueleza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia
Suluhu Hassan kuhusu wakulima wa kuzalisha Mbegu za Mpunga kwenye
Bonde la Kinyasini -kisongoni Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakati wa
Ziara ya kutembelea Miradi ya Tasaf na Assp inayofadhiliwa na serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema Serikali imekua ikitoa pesa nyingi
kufadhili wana nchi katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwalengo kwamba
wananchi hao waweze kujikwamua na umasikini na kujipatia kipato jambo ambalo
baada ya mradihuo kukabidhiwa wananchi husuasua na hatimae kufa kituambacho
hakifurahishi.
Amesema wana nchi wajifunze kuituza na
kuendeleza miradi hiyo kwani ina umuhimu mkubwa na kuwanufahisha wao wenyewe.
“kuiacha miradi ife sivizuri ,muichangie
iliijiwezekujiendesha na huko ndio faida ya miradi hiyo”.alisema Samia.
Aidha Waziri aliwambia wakulima wa bonde la
jendele Kinyasini Kisongoni wajitume kwa kuzalisha kwa wingi chakula kwani sasa
hakuna sababu kwavile maji yapo ya kutosha katika bonde hilo hivyo
uzalishaji ungezeke.
Waziri hoyo alisema dhamira ya ziara yake
kuja Zanzibar
ni kuona vipi matumizi ya pesa za TASAF zinavyo tumika katika miradi ilio
ombewa na utekelezaji wake umefikiaje kwa wananchi.
Waziri alifurahishwa na juhudi zinazo
chukuliwa kwani kumefikiwa hatua kubwa za kumaendeleo na zinatia moyo kwa
matumaini .
Waziri alitembelea mradi wa mpunga wa umwagiliaji maji jendele na mradi
wa uzalishaji mbegu za mpunga kinyasini kisongoni na badae kupata maelezo juu
ya miradi ASSP na SPDL inayo endeshwa na wizara yakilimo na maliasili na ushirika
Zanzibar .
Miradi hiyo kwa TASAF ya awamu ya kwaza Zanzibar ilipatiwa dola za kimarekani milioni tatu
ambapo ziligawiwa sawa sawa kwa unguja na pemba.
Awamu ya pili TASAF Zanzibar ilipatiwa dola
za kimarekani 2,500.000.00 ambapo
zilitumika kumalizia mradi wa kwaza unguja na pemba kupitia mifuko mitatu nayo
ni mfuko wa Taifa wa kijiji (NVF) wenye thamani ya fedha TShs
2,500,000,000.00,mfuko wa mradi wa ukanda wa Bahari (MACEMP) wenye thamani ya
fedha TShs 1,800,000.000.00
-Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan
akipita kwenye shamba la mpunga la kuzalishia Mbegu
la kinyasini-kisongoni Walaya ya Kaskazini A Unguja Waziri akiwa katika
Ziara ya kutembelea Miradi iliyofadhiliwa na ASSP [Picha na Ali Meja ]
No comments:
Post a Comment