header

nmb

nmb

Thursday, April 5, 2012

Habari kamili kuhusu Lema kuvuliwa ubunge hizi hapa









Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini, Lema

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemvua ubunge, aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini, Godbless Lema.


Mahakama hiyo imetoa uamuazi huo katika hukumu ya kesi iliyokuwa inamkabili Lema ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ambao ulimpa ushindi Lema.


Katika kesi hiyo iliyofunguliwa na wanachama watatu wa CCM, ilimlalamikia Lema kuwa alitoa matamshi ya matusi na kejeli dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Matilda Salha Burian.


Hukumu imetolewa leo na Jaji Gabriel Rwegabrila wa Sumbawanga, huku umati wa watu ukisubiri kwa shauku za namna mbalimbali.


Kwa mujibu wa habari kutoka Arusha, baada ya hukumu hiyo, Lema amesema fursa ya kukata rufani aliyopewa na mahakama hiyo, hataitumia badala yake, anasubiri kuingia tena kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi itakapopiga kipyenga.


Lema amesema, uamuzi wa mahakama amekubaliana nao, na kilichobaki anasubiri uamuzi wa wananchi wenyewe wa Arusha, badala ya kutaka awe mbunge wa mahakamani.

No comments:

Post a Comment