header

nmb

nmb

Tuesday, April 10, 2012

0 Comments
Steven Kanumba.
Florence Majani na Suzzy Butondo wa gazeti la Mwananchi

MSANII nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu zimeeleza.

Taarifa hizo za ndani, zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya saa mbili.

“Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi…

UPDATES ZA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA VIWANJA VYA LEADERS LEO

Posted by GLOBAL on April 10, 2012 at 10:30am 0 Comments
Steven Charles Kanumba "The Great".
Kwa sasa mwili wa marehemu umewasili katika Viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam, na ibada ya kumuaga inaendelea. Mwili wa marehemu umepokelewa Viwanja vya Leaders ukitanguliwa na mapokezi ya wazazi wake, viongozi mbalimbali wa serikali ambao juu yao kabisa alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal.
Saa 4:49 asubuhi: Ratiba ya mwanzo imebadilika kidogo, kwa sasa baadhi ya viongozi wa serikali wanaaga mwili wa marehemu ili waweze kupata fursa ya kuendelea na…

RATIBA YA KUMUAGA MPENDWA WETU STEVEN CHARLES KANUMBA "THE GREAT" VIWANJA VYA LEADERS LEO

Posted by GLOBAL on April 9, 2012 at 3:00pm 3 Comments

KAMATI YA MAZISHI YA MSANII STEVEN CHARLES KANUMBA
    Taarifa kwa vyombo vya habari
        APRILI 9, 2012

Msanii wa filamu, aliyebeba mapenzi makubwa ya Watanzania, Waafrika na dunia kwa jumla, Steven Charles Kanumba aliyefikwa na mauti ghafla Aprili 7, 2012, atazikwa kesho Makaburi ya Kinondoni,…

STEVEN CHARLES KANUMBA KIMYA MILELE

Posted by GLOBAL on April 10, 2012 at 9:00am 0 Comments
Steven Charles Kanumba enzi za uhai wake.
Mama Mzazi wa Steve Kanumba, Bi. Flora Mgoa akiwa na Simanzi kubwa.
Irene Uwoya akilia kwa uchungu.…

LULU: NAOMBA MNISAMEHE

Posted by GLOBAL on April 10, 2012 at 9:21am 0 Comments
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Marehemu Steven Charles Kanumba "The Great" wakati wa uhai wake.
Na Shakoor Jongo

MSANII wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye yupo mahabusu katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es Salaam, amesema anaomba msamaha kwa Watanzania kutokana na kifo cha muigizaji maarufu nchini, Steven Kanumba aliyefariki…

WEMA: SIJAWAHI KUACHANA NA KANUMBA

Posted by GLOBAL on April 10, 2012 at 9:28am 0 Comments
Wema Sepetu akiwa na Steve Kanumba enzi za uhai wake.
Na Shakoor Jongo

SIKU chache baada ya kifo cha muigizaji mkubwa katika tasnia ya filamu Bongo, marehemu Steven Charles Kanumba, Miss Tanzania 2006/07, Wema Sepetu amefunguka kuwa hakuwahi kuachana na muigizaji huyo.

Akizungumza kwa sauti iliyoambatana na kilio cha kwikwi katika mahojiano maalumu na kituo kimoja cha redio nchini, Wema alisema kuwa ingawa jamii ilikuwa ikifahamu kuwa ameachana naye, ukweli ni kwamba bado walikuwa wapenzi kwa siri.

“Tulikuwa na mapenzi ya siri kati yetu na tulifanya hivyo kwa kuwa kila…

DUNIANI HADI KUZIMIKA GHAFLA

Posted by GLOBAL on April 10, 2012 at 9:34am 0 Comments

Na Elvan Stambuli

MWIGIZAJI nguli Tanzania, Steven Kanumba amefariki dunia au kuzimika ghafla nyumbani kwake maeneo ya Vatican Sinza, jijini Dar es Salaam usiku wa Jumamosi. Hii hapa ni historia yake kwa ufupi.

HISTORIA YAKE:

Steven Charles Kanumbaa alizaliwa Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga kabla ya umauti kumfiia Aprili 7, mwaka huu. Ni mtoto wa tatu katika familia yako akiwa na dada zake wawili.

Elimu ya msingi alipata katika Shule ya Bugoyi na baadaye akajiunga na  Sekondari ya Mwadui, kabla ya kuhamia Dar Christian Seminary.

Baada ya kumaliza kidato cha nne Dar Christian Seminary, Kanumba alijiunga na Sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam kwa elimu ya kidato cha tano na Sita.

No comments:

Post a Comment