header

nmb

nmb

Wednesday, February 8, 2012

MSAADA JAMANIMKAZI WA FRELIMO IRINGA ESTHER MAGINGA AOMBA MSAADA KUTIBIA KANSA YA TITI


*Mkazi wa Frelimo Manispaa ya Iringa, Esther Maginga (60) ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya titi toka mwaka 1996 anawaomba wasamaria wema popote nchini na duniani kujitokeza kumsaidia kuokoa maisha yake kutokana na tatizo la kansa ya titi linalomsumbuka .
Mwanamke huyo mwenye familia ya watoto sita amesema kuwa ameamua kujitokeza na kuomba msaada huo kutokana na mumewe kutokuwa na uwezo wa kifedha kuweza kumsaidia kutokana na shughuli yake ya gereji ambayo huishia kupata fedha za chakula na kodi ya nyumba tu.Hivyo alisema hata watoto wake wamekuwa wakiishi kwa msaada wa wasamaria wema ambao wamekuwa wakimsaidia kuwasomesha watoto hao elimu ya sekondari.Aidha alisema kuwa ili kufanikisha kwenda Hospitali ya taifa ama KCMC kwa ajili ya matibabu ni kiasi cha shilingi milioni 2.5 zinahitajika na kuwaomba wasamaria wema kumsaidia ili kunusuru maisha yake kutokana na sasa hali ya uvimbe katika titi kuanza kuongezeka zaidi.Kwa wale watakao guswa kuungana na mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com kwa ajili ya kusaidia kuokoa maisha ya mtanzania mwenzetu huyo waweza kutumia huduma ya M-PESA kwa namba 0754 026 299 ama tigo Pesa kwa namba 0712 750199 na Mungu atakubaliki kwa mchango wako.

No comments:

Post a Comment