header

nmb

nmb

Wednesday, February 8, 2012

BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) LAHAIRISHA KESI DHIDI YA KATIBU MKUU WA WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO JOYCE MAPUNJOKatibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Joyce Mapunjo akielezea jinsi alivyodhalilishwa na gazeti la Dira ya Mtanzania mbele ya Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) wakati kesi hiyo iliyoendeshwa jijini Dar es Salaam.


Mhariri wa Habari wa gazeti la Dira ya Mtanzania, Ponsian Rwechungura akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) wakati wa usikilizwaji wa shauri la Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Joyce Mapunjo dhidi ya gazeti la Dira ya Mtanzania.


Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya MCT Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akiahisha shauri hilo.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Joyce Mapunjo (kulia) wakiwa na Mhariri wa Habari wa gazeti la Dira ya Mtanzania, Ponsian Rwechungura wakifuatilia maamuzi Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) wakati wa usikilizwaji wa shauri lao.


Wasikilizaji wakifuatilia shauri.


Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania wakati wa usikilizwaji wa shauri la Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Joyce Mapunjo dhidi ya gazeti la Dira ya Mtanzania.

Kesi ya udhalilishaji wa kihabari iliyofunguliwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Joyce Mapunjo dhidi ya gazeti la Dira ya Mtanzania, imeahirishwa mpaka wakati mwingine baada ya uongozi wa gazeti hilo kushindwa kumleta mhusika halisi wa kujibu tuhuma zinazolikabili gazeti hilo, mbele ya Mahakama ya usuruhishi ya Baraza la Habari nchini MCT.


Akizungumza mara baada ya kuahirisha kesi hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya MCT Jaji Mstaafu Thomas Mihayo aliutaka Uongozi wa gazeti hilo kuhakikisha unamleta kiongozi husika anayefahamu vizuri chimbiko la tuhuma hizo, ili kuepusha matatizo zaidi endapo katibu mkuu huyo atapewa ruhusa ya kulifikisha suala hilo mahakani.
Katika hatua nyingine Baraza hilo limeahirisha kesi nyingine ya udhalilishaji iliyofunguliwa na Waziri mkuu mstaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Edward Lowasa dhidi ya gazeti hilo kutokana na Kiongozi huyo kuwepo bungeni mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment