header

nmb

nmb

Thursday, January 26, 2012

TAARIFA ZAIDI ZA MBUNGE MBUNGE MSTAAF, GALINOMA AFARIKI DUNIA
Marehemu Stephen Galinoma
Habari za uhakika zilizotua katika mtandao huu kutoka Kalenga katika wilaya ya Iringa vijijini zinadai kuwa mbunge wa zamani wa jimbo la Kalenga Mhe.Stephen Galinoma pichani amefariki dunia asubuhi ya leo wakati akikimbizwa katika hospitali teule ya wilaya ya Iringa ya Ipamba .
Habari ambazo mtandao huu umezipata na kuthibitishiwa na mtoto wa Galinoma Magreth zinadai kuwa Galinoma amefariki majira ya asubuhi wakati akikimbizwa hospital hiyo ya Ipamba .
Alisema kuwa marehemu kabla ya kifo chake alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo na taarifa zaidi utaendelea kuzipata katika mtandao huu .
Marehemu Galinoma alikuwa mbunge wa jimbo la Kalenga kupitia CCM kuanzia mwaka 2005 hadi 2010 alipostaafu na nafasi yake kuchukuliwa na mbunge wa sasa Dr Wiliam Mgimwa .

No comments:

Post a Comment