header

nmb

nmb

Monday, January 9, 2012

Jeuru ya Boko Haram, wanamizizi serikalini'

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan kwa mara ya kwanza amesema anahofia kuwa kundi hilo la waislamu wenye msimamo mkali wanaungwa mkono na baadhi ya maafisa wa usalama na wakuu wa serikali.kanisa Nigeria

Wakristo ndio wanaolengwa


Rais Jonathan amesema hayo kufuatia mashambuizi ya hivi karibuni nchini humo ambapo watu 80 wameuawa na mali ya mamilioni ya dola kuharibiwa.
Kiongozi huyo amesema hali ya usalama nchini humo sasa ni mbaya na ya kutatiza kuliko wakati wa vita vya wenyewe kwa wenye vilivyoshuhudiwa nchini humo kati ya mwaka wa 67 na 70.


Wakati wa vita hivyo zaidi ya watu milioni moja waliuawa.


Mamia ya watu hasaa wakristo wamelazimika kuhama mkaazi yao kufuatia mashambulio yaliodumu saa 24 wiki iliopita yaliotekelezwa na makundi ya watu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa Boko Haram.


Kundi hilo la Boko Haram lina lengo la kuipindua serikali na kuteua utawala wa kiislamu nchini Nigeria.


Akizungumza wakati wa Ibada katika kanisa la Rememberance Day mjini Abuja, Rais Jonathan alisema usalama nchini humo upo katika hali mbaya sana kwa kuwa imekuwa vigumu kumtambua adui.


"wengine wapo serikali, kwenye jeshi, polisi na hata kwenye idara ya mahakama, hali ni mbaya sana, ata ikiwa mtoto wako ni mwanachama wa kundi hilo hauwezi kujua" alisema kiongozi huyo.


Viongozi wa kikristo wanailaumu serikali kwa kutowalinda dhidi ya mashambulio hayo yanayowalenga.


Wiki iliopita Rais Jonathan alitangaza hali ya hatari katika majimbo ya Yobe, Borno, Plateau na Niger kufuatia mashambulizi hayo. habari ya BBC


No comments:

Post a Comment