header

nmb

nmb

Tuesday, January 10, 2012

MAMBO YA DAR LIVE KILA WIKIENDI!
Kiongozi wa wanenguaji wa Extra Bongo, Hassani Mussa ‘Super Nyamwela’ akiserebuka na mashabiki zake.
Mwimbaji wa kundi la East Africa Merodi’, Mwanahawa Ally, akitumbuiza.

Mnenguaji wa Bendi ya Extra Bongo ‘Next Level’, Otilia Boniface, akiwajibika.
Chege akiwajibika kwa staili yake.

Wasanii wa kundi la Wanaume Family Chege na Temba wakifanya makamuzi jukwaani.
Temba, akijinafasi na mrembo.
Mnenguaji wa Etra Bongo, Mwantum Juma, akimkatikia shabiki wake.
Hassani Mussa ‘Super Nyamwela’ (Kushoto) akinengua na mnenguaji mwenzake.
Mashabiki wakijinafasi na kundi la East Africa Melody Taarab.
Mashabiki wakiwa kazini.

Mtu mzima akiwajibika na mrembo…
Mambo ya Pwani hayo.
Mwanamuziki wa Bendi ya Extra Bongo ‘Next Level’, Banza Stone, akiwa jukwaani.
Dogo Aslay akionyesha uwezo wake.
…Akiwa amembeba Dogo Mo baada ya kuimba.

Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Next Level’, Ali Choki, akiimba kwa hisia kali.
Watoto wakiogelea.
Mashabiki wakifuatilia burudani ukumbini hapo.

KITONGOJI cha Mbagala jijini Dar es Salaam kiligwaya kwa furaha kutokana na uhondo wa muziki ulioangushwa katika kituo cha burudani cha Dar Live ambapo waliojimwaga hapo walikonga nyoyo zao kwa muziki wa aina mbalimbali ukiwemo wa kizazi kipya na muziki wa dansi na taarab.

Miongoni mwa wasanii waliokuwa hapo ni pamoja na kina Chege, Temba kutoka kundi la Wanaume Family, bendi ya Extra Bongo, East Africa Melody Taarab, kundi la JNY Unit na kundi la Mkubwa na Wanaye linaloongozwa na Said Fella ambalo lilisheheni wanamuziki kama Mwalami Hamisi (Dogo Mo) na Aslay Isihada (Dogo Asley).

Habari/Picha: Musa Mateja/GPL.

No comments:

Post a Comment