header

nmb

nmb

Tuesday, January 10, 2012

MSANII DIAMOND CHUPUCHUPU KUFUNGWA JELA




MAMIA wafurika kushuhudia hukumu ya msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Naseeb Abdul a.k.a Diamond akihukumiwa kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya shilingi elfu 50.000 kwa kosa la kumshambulia na kuharibu mali za mwandishi wa habari mkoani Iringa Francis Godwi.





Hatua hiyo imekuja baada ya msanii Diamond na wacheza shoo wake wawili kukiri kosa mbele ya mahakama yeye na wenzake kwa kuharibu Camera mbili, Lap top aina ya Accer pamoja na kumshambulia mwanahabari Francis Godwin Desemba 31 mwaka jana katika uwanja wa Samora mjini Iringa.


Akitoa hukumu hiyo hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Hakimu Masua alisema kulingana na watuhumiwa wote watatu kukiri kosa hilo anawahukumu kwenda jela miezi 6 au kulipa fidia ya shilingi elfu hamsini kila mmoja na huku wakilazimika kumlipa Godwin shilingi elfu 30 kila mmoja na kufanya kufikia kiasi cha shilingi 90000 Wakitoa utetezi wao watuhumiwa hao walisema mahakama iwapunguzia adhabu kwa kuwa hawakukusudia kufanya kosa hilo, na wao walikuja mkoani hapa kwa ajili ya kutoa burudani, na kuwa tukio hilo wamelifanya kwa ghadhabu.

No comments:

Post a Comment