header

nmb

nmb

Tuesday, January 24, 2012

KESI YA DAVID MATTAKA NA QWNZAKEYAHAIRISHWA MPAKA FEBRUARI 23, 2011




Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, leo imeshindwa kumsomea maelezo ya awali, yaani PH, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka na wenzake wawili kutokana na mawakili wa upande wa utetezi kushindwa kufika mahakamani hapo.


Mataka anakabiliwa na makosa matatu likiwemo kosa la matumizi mabaya ya madaraka kinyume na Sheria na kifungu 31 Na.11 ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007.


Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kaimu Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha Elisaph Mathew Ikomba na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Ndani, William Haji.


Katika shtaka la kwanza linalowahusu washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kuwa walishindwa kutunza kumbukumbu za mawasiliano ya manunuzi waliyokuwa wakifanya na mtoa huduma kinyume na kifungu cha 55 (3), 87 (1) (f) cha Sheria ya Manunuzi ya Umma Na. 21 ya mwaka 2004 na kanuni ya 17(1) ya Sheria ya Manunuzi (Goods, Works, Non-Consultant Services and Disposal of Public Asets by Tender) Regulation, G.N. No.97 of 2005.


Upande wa mashtaka unadai shtaka la pili ambalo pia linawakabili washtakiwa wote ni la kushindwa kutimiza matakwa ya vifungu vya Sheria ya Manunuzi ya Umma na Kanuni zake kinyume na kifungu cha 87 (1) (f) cha Sheria ya Manunuzi ya umma ya mwaka 2004.


Shtaka la tatu linalo mkabili Mattaka pekee linahusu matumuzi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa ya mwaka 2007


Mara tu baada ya kesi hiyo kuanza, mapema leo asubuhi upande wa mashtaka ukiongozwa na mwendesha mashtaka kutoka TAKUKURU, BENY LINCOLYNE, ulieleza kuwa uko tayari kwa ajili ya kesi hiyo ambapo hata hivyo hakimu , RITTA TARIMO alilazimika kuiahirisha mpaka Februari 23 mwaka huu baada ya kuona kwamba mawakili wa utetezi hawakuwemo katika chumba cha mahakama ilikokuwa ikiendeshwa kesi hiyo.


No comments:

Post a Comment