header

nmb

nmb

Tuesday, January 24, 2012


SUMA LEE, AT, MASHAUZI CLASSIC , MASHUJAA, EXTRA BONGO WAKAMUA DAR LIVE .

Mkurugenzi wa kundi la Mashauzi Classic Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’, akiwajibika.


Extra Bongo chini ya Ally Choki (wa pili kushoto), wakiwajibika.


.Mkurugenzi wa kundi la Mashauzi Classic Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’,Akijinafasi jukwaani.


Msanii anayetamba na ‘Hakunaga’, Ismaili Thabit ‘Suma Lee’, akiwajibika na mcheza shoo wake aliye tikisa sana katika albam hiyo.


…..Suma Lee akiserebuka na mkali wa miondoko ya kwaito.


…..Akikamua na mmoja wa wanenguaji wake.


Ally Tall ‘AT’ akiwa amekaa chini baada ya raha kumkolea wakati wa makamuzi.


Nyota wa bendi ya Mashujaa, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ akikamua na wanenguaji wake katika jukwaa la kisasa zaidi.


Wanenguaji wa Extra Bongo wakifanya kazi jukwaani.


Wakali Dancers wakipagawawisha.


Wasanii wa kundi la Sliders wakionyesha uwezo wao.


Watoto Wakichorwa mapambo usoni


Watoto Wakilishwa keki na kipande cha nyama wakati wa kutoka ukumbini humu ikiwa ishara ya upendo wa uongozi wa ukumbi huo.

-----

WASANII wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Ismaili Thabit ‘Suma Lee’, Ally Tall ‘AT’, Mashauzi Classic, Extra Bongo ‘Next Level, na Bendi ya Mashujaa usiku wa kuamkia leo walipata nafasi ya kufanya makamuzi ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam.Wasanii hao waliwapagawisha mashabiki wa pande hizo na wakausifia Dar Live wakisema kuwepo kwake kulikuwa mwanzo wa wao kufanya shoo za kimataifa huko Mbagala.


Miongoni mwa wasanii hao waliotumbuiza hapo kwa mara ya kwanza tangu ufunguliwe Januari Mosi mwaka huu, waliahidi kupiga shoo zaidi pindi wanapoalikwa.Shoo hiyo pia ilisindikizwa na kundi la wanenguaji la Sliders kutoka Kinondoni jijini Dar na Wakali Dancers la Temeke ambao pia walifanya makamuzi ya kufa mtu na kusifia mandhari ya ukumbi huo. (HABARI PICHA KWA HISANI YA BLOGU YA HAKI NGOWI)

No comments:

Post a Comment