Baada ya Serikali kutoa msimamo wake juu ya masharti ya Serikali ya Uingereza kutoa misaada kwa nchi masikini ikiwamo Tanzania, ziara ya mtoto wa Malkia wa Uingereza, Elizabeth II, inatarajiwa kupokewa na mabango ya kupinga masharti hayo.
Prince Charles na mkewe Camilla, wako hapa nchini tangu jioni ya jana kwa ziara ya siku nne nchini, ambapo wanaharakati nchini wamepanga kumpa ujumbe wa kupinga masharti ya misaada kwa kulinda haki za mashoga nchini.
Waandamanaji wenye mabango kwa mujibu wa habari zilizopatikana jana Dar es Salaam, watajipanga katika maeneo atakayotembelea mgeni huyo, wakiwa na mabango yanayounga mkono kauli ya Serikali kulaani tishio la Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, la kukata misaada kwa nchi ambazo hazitaruhusu ushoga.

No comments:
Post a Comment