header

nmb

nmb

Monday, September 12, 2011

MBANDIKA MABANGO WA CCM AFANYIWA KITENDO CHA KIKATILI IGUNGA.

MFUASI wa CCM, Mussa Tesha (24) akiwa katika hospitali ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, leo. Tesha ameungua usoni na sehemu kadhaa mwilini baada ya kumwagiwa tindikali usiku wa kuamkia leo na watu wasiofahamika , ambapo inaelezwa kuwa walimwagia tindikali hiyo alipokuwa katika harakati za kubandika mitaani mabango ya mgombea wa Ubunge jimbo lgunga kwa tiketi ya CCM. Tesha alitarajiwa kuhamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Sala leo kwa gharama za CCM
KAPINGAZ Blog inavilaani sana vitendo vya watu wanaoivamia Siasa na kufanya vitendo vikatili kama hivi. Napenda niwaombe wana Blog wenzango tuvilaani kwa nguvu kubwa kwa sababu tukivikalia kimya vinaweza kuwakuta na wenzetu wanaotoa habari za uchaguzi huko Igunga na sehemu nyingine.kunako fanyika chaguzi kama hizi.

No comments:

Post a Comment