header

nmb

nmb

Thursday, July 8, 2010

PIKIPIKI YA MCHINA YAUA!!




DEREVA wa Pikipiki Omaer Mfaume (21),mkazi wa Kitunda kati amefikishwa Mahakamani akikabiliwa na shitaka la kuua mtu baada ya kumgonga na pikipiki.

Mshitakiwa huyo amesomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Janet Kinyage wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala.

Imedaiwa na Mwendesha Mashitaka Inspekta Mussa Gumbo kuwa tukio hilo lilitokea Juni 17 mwaka huu,Kitunda.

Inspekta Gumbo amedai kuwa mshitakiwa akiwa dereva aliendesha pikipiki yenye namba za usajili T 483 BDY bila uangalifu katika barabara ya uuma na kumgonga Julius Msiwa na kusababisha kifo chake.

Mshitakiwa alikana shitaka hilo na kesi yake itatajwa tena Agosti 26 mwaka huu.

Wakati huo huo, Faida Ngurumo (24),mkazi wa KImara Baruti amefikishwa katika Mahakama hiyo akituhumiwa kwa wizi wa pikipiki.

Upande wa Mashitaka ukiongozwa na Inspekta Mussa Gumbo ulidai mbele ya Hakimu Janet Kinyage kuwa wizi huo ulitokea Julai 2 mwaka huu,saa 11 alfajiri,Upanga.

Amedai kuwa mshitakiwa aliiba pikipiki aina ya Chuma yenye thamani ya sh.1,800,000 mali ya ramadhan Omar.

Mshitakiwa amekana shitaka na kesi yake itatajwa tena Julai 20 mwaka huu.
By Saida Said wa Dar leo

No comments:

Post a Comment