header
nmb
Thursday, July 8, 2010
MWANAMKE AJINYONGA KWA KUTELEKEZEWA WATOTO SITA NA MUMEWE!!
PICHANI KUSHOTO NI MWANAHARAKATI WA KUTETEA HAKI ZA WANAWAKE NCHINI BI. ANANILEA NKYA AKIPOKEA TUZO.
MWANAMKE Sauda Mussa (36) mkazi wa Arusha amekufa baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani kwa kile kilichodaiwa ni kutokana na kushindwa kuwalea watoto sita baada ya mumewe kumtelekeza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Basilio Matei amesema kuwa tukio hilo limetokea jana saa 5 asubuhi, katika kijiji cha Qwandet, Kata ya Mang'oa wilayani Karatu.
Amesema kuwa mume wa marehemu ametambulika kwa jina Fadhili Saidi (46) ambaye anatuhumiwa kumtelekeza mkewe na kwenda kuishi na wanawake wengine kwa kipindi cha miezi sita.
Kamanda amesema kuwa kutokana na kitendo hicho mwanamke huyo alikuwa akiwatunza watoto hao peke yake huku akijishughulisha na kilimo.
Imedaiwa kuwa mwanamke huyo hakuweza kumudu kuitunza familia hiyo kutokana na watoto hao kukosa sare za shule na pia kushindwa kumudu kulipa ada za shule.
Imedaiwa kuwa kutokana na hayo mwanamke huyo aliamua kukatisha uhai wake kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani nje ya nyumba aliyokuwa akiishi jana asubuhi.
Hata hivyo imedaiwa kuwa mwanaume huyo amekuwa na tabia ya kuwazalisha wanawake na kushindwa kuwalea watoto.
"Inadaiwa kuwa mwanaume huyu aliondoka katika mazingira ya kutatanisha na sasa ana wake wanne katika vijiji tofauti, " amesema.
Kamanda Matei amesema kuwa kabla ya uhai wake marehemu aliwahi kunywa sumu lakini majirani walifanikiwa kumwokoa kwa kumpeleka hospitali.
By. Rehema Maigala na Stela Aron. toka kwa RPC ARUSHA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment