WACHEZAJI wa timu ya Taifa ya Ghana 'Black Stars' wamezawadiwa kitita cha dola 20,000 kila mmoja kutokana na kufanya vizuri katika Fainali za Kombe la Dunia 2010 zinazoendelea nchini Afrika Kusini.
Ghana waliaga michuano hiyo katika hatua ya robo fainali baada ya kutolewa na Uruguay kwa penalti 4-2 na kuwa timu ya mwisho ya kutoka katika michuano hiyo.
Kwa mujibu wa Rais wa Nchi za Magharibi, Professa John Atta-Mills, alisema mbali na wachezaji lakini kipa kiongozi aliyekuwa katika benchi la ufundi la timu hiyo na viongozi wa Chama cha soka nchini humo watapata dola 10,000 kila mmoja.
Mabingwa hao wa Afrika kwa mara nne walijitahidi kwa kila hali kuliwakirisha vizuri bara la Afrika katika michuano hiyo kabla ya ndoto zao za kutwaa ubingwa Dunia kuyeyuka katika hatua hiyo ya robo fainali.
“Hawajatwaa Kombe la Dunia lakini kutokana na kiwango walichoonesha katika michuano hiyo hawakupeperusha bendera ya Ghana pekee bali bara zima la Afrika,” Rais Mills alisema.
Rais huyo aliongeza: “Tumekuwa tukiisapoti Ghana mwanzo na sasa tunatakiwa kuendelea kuisapoti kutokana na uwezo wao waliouonesha katika michuano hiyo na kuiweka Ghana pale ilipostahili kuwa".

No comments:
Post a Comment