UMATI mkubwa umekusanyika leo asubuhi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Nkoaranga wilayani Arumeru baada ya bibi harusi kutoweka katika mazingira ya kutatanisha na kukutwa mtoni akiwa hajitambui.
Tukio hilo limetokea Jumamosi usiku mkoani Arusha baada ya bibi harusi huyo, Christina Joseph (29), kufunga ndoa na mumewe, Daniel Ayali.
Imedaiwa kuwa baada ya kumaliza tafrija yao wana ndoa hao walikwenda kulala hotelini ambapo bibi harusi alikwenda kuoga lakini bwana harusi alishikwa na butwaa baada ya mkewe kuchelewa kutoka.
Kutokana na hali hiyo bwana harusi aliamua kumfuata ambapo alikuta maji ya bomba la mvua yakiendelea kutoka na yeye kutoonekana.
Imedaiwa kuwa bwana harusi aliamua kumtafuta kila kona lakini hakuweza kumwona na kuamua kutoa taarifa kwa wazazi wa pande mbili pamoja na kanisani.
Kutokana na hali hiyo, Jumapili mchungaji wa usharika huo, aliyefahamika kwa jina moja la Ananieli kwa kushirikiana na ndugu walianza kufanya maombi kwa siku nzima.
Kwa mujibu wa ndugu, mchungaji huyo amesema kuwa bibi harusi huyo alipatikana jana saa 3 asubuhi katika bonde la Mto Meru akiwa mtupu na hajitambui.
Amesema walipata taarifa kutoka kwa ndugu ambao walikwenda kwenye mto huo kwa shughuli mbalimbali na kuja kuchukuliwa.
Hata hivyo, wakati wakiendelea na maombi ghafla mwanamke mmoja alidondoka kanisani hapo akiwa amevaa kaniki nyeusi na ameshika vibuyu.
Katika mahojiano alidai kuwa yeye ndiye aliyemchukua bibi harusi na kuwa alifanya hivyo kutokana na kutaka mtoto wake aolewe na bwana harusi huyo.
.ZAIDI NUNUA DAR LEO YA LEO

No comments:
Post a Comment