MGOMBEA urais kwa tiketi ya chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Muttamwega Mgaywa, ametema cheche zake jana katika Mkutano Mkuu wa chama hicho na kuwaeleza wajumbe wa Halmashauri Kuu kuwa katika kampeni zake atatumia usafiri wa ndege na kwamba mpaka sasa ana helkopta mbili na magari ya kumwaga.
Akizungumza wakati alipokuwa akijinadi ili achaguliwe, Mgaywa alisema yeye siyo mtu wa wasiwasi na kwamba alikuwa akifanya kazi ya umachinga na kwamba ni kada mwaminifu wa chama hicho kwa muda mrefu.
“Mimi katika kampeni zangu nitatumia helkopta ambayo nitapanda na mwenyekiti wangu pamoja na baadhi ya wajumbe kuzunguka nchi nzima. Magari siyo tatizo ninayo ya kumwaga kwa hiyo nimejiandaa ipasavyo,” amesema.
Amesema lengo kubwa ni kuhakikisha kwamba anafanya kampeni zitakazokuwa na mafanikio makubwa katika chama hicho ili kuhakikisha kwamba wanapatikana wabunge na madiwani wengi mwaka huu na wala si vinginevyo.
Mgaywa amesema katika mikoa na wilaya zote atakazopita atahakikisha kwamba anapeperusha bendera ya chama hicho pamoja na kusimamisha ofisi nchi nzima na kuwataka wajumbe kumpa ushirikiano.
Amesema kama atachaguliwa kuwa rais atahakikisha kuwa anashirikiana na wapinzani wote na kwamba pale atakapopita katika kampeni na kuona kuwa kuna chama cha upinzani kina nguvu ataakikisha kwamba wanashirikiana ili kiweze kupata viongozi wengi. IMEANDIKWA NA G. MBOMA .

ZAIDI GAZETI MAKINI LA MCHANA DAR LEO YA LEO
No comments:
Post a Comment