header

nmb

nmb

Thursday, June 17, 2010

MTOTO ALIYEPOTEA KWA TUHUMA ZA UCHAWI APATIKANA!!

SANGOMA WAIBA WATOTO
HATIMAYE mtoto Deogratus Jumanne (6) aliyekuwa amepotea wiki mbili zilizopita na kusababisha familia kufikishana kwa sangoma, amepatikana huku akiwa amejeruhiwa.
Mtoto huyo aliyepatikana akiishi katika nyumba za askari katika barabara ya Kilwa baada ya kuokotwa maeneo ya Mbagala.
Kupatikana kwa Deogratus kulitokana na taarifa zilitolewa wiki iliyopita na gazeti hili na kusababisha polisi hao kupata taarifa kupitia vyombo vya habari.
Polisi hao waliamua kupiga simu kwa baba mzazi wa Deogratus, Jumanne Loki (48) mkazi wa Kiwalani na kumtaka kufika kituo cha Polisi Kilwa ili kumtambua mtoto wake.
Loki alikabidhiwa mtoto wake na kuelezewa hali halisi alivyokutwa kwa tuhuma za kupigwana mama wa kambo jambo lililozua tafrani kwa familia hii.
Akizungumza na gazeti hili baba mzazi wa mtoto huyo, Loki amesema kuwa amesikitishwa na kitendo hicho hivyo wamepewa PF3 kwa ajili ya kumchunguza afya yake.
Awali ililipotiwa kwamba mtoto Deogratus aliondoka nyumbani kwao Kiwalani Mei 20 mwaka huu na kwenda kwa bibi yake lakini baada ya siku tatu alilipotiwa kupotea ambapo taarifa zilitolewa kituo cha Kizuiani Maturubai na kupewa RB MBL/RB/4580/10.
Habari zaidi,Dar Leo ya leo.

No comments:

Post a Comment