RAIS WA ZAMBIA
MFUKO wa Kimataifa wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria umesitisha msaada wenye thamani zaidi ya dola milioni 300 za Marekani kwa sekta ya afya nchini Zambia kwa kile ulichodai ni tuhuma za rushwa zilizokithiri katika sekta hiyo.
Msemaji wa Shirika hilo ameliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa badala yake fedha hizo zitaelekezwa katika sekta nyingine.
Hii siyo mara ya kwanza kwa Zambia kusimamishiwa misaada kama hiyo ikihusishwa na tuhuma za rushwa baada ya siku za nyuma Sweden na Uholanzi kuchukua hatua kama hiyo huku Umoja wa Jumuiya ya nchi za Ulaya EU ikisitisha msaada wake kwa ajili ya ujenzi wa barabara.
Mkurugenzi wa Mawasiliano katika mfuko huo, John Liden, ameiambia BBC kuwa mpango wa kuokoa maisha hautaguswa.
Amesema mfuko huo umefikia hatua hiyo baada ya Zambia kushindwa kuchukua hatua muhimu tangu vitendo hivyo vya rushwa viripotiwe kwa mara ya kwanza.
“Tuliibaini idadi kubwa ya wahusika na tukaitaarifu serikali ya Zambia kuhusu jambo hilo,” amesema.
“Tuliendelea kuwaagiza kuchukua hatua lakini kukawepo na utendaji hafifu kwa upande wa Zambia na hii ndiyo moja ya sababu ambayo tunadhani hatuna imani na Wizara ya Afya na katika hatua hii hatuwezi kuendelea kutoa misaada kwa ajili ya sekta ya afya Zambia,” aliongeza.
Mwandishi wa BBC amesema uamuzi huo utakuwa pigo kubwa kwa Serikali ya Zambia ambayo inategemea misaada kuhudumia waathirika wa Virusi vya UKIMWI.
Miaka mitano iliyopita mfuko huo pia ulisimamisha misaada yake kwa Serikali ya Uganda kwa kushindwa kusimamia kwa udhabiti misaada yake.
Shirika hilo ambalo lilianzishwa mwaka 2002 chini ya maagizo ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN, Kofi Annan umekwishasambaza zaidi ya dola bilioni 19 kwa ajili ya kupambana na UKIMWI,Kifua Kikuu na Malaria.
Hata hivyo, mwandishi wa BBC anayeshughulikia masuala ya ulimwengu, Adam Mynott amesema kuwa misaada hiyo inatia shaka kama inawafikia walengwa na akasema kwamba inakadiliwa kuwasaidia watu milioni tano tu.
Misaada hiyo ambayo inatoka Serikalini na vyanzo binafsi imekuwa ikielekezwa katika mataifa maskini ulimwenguni na mwandishi wa BBC anasema kuwa mengi ya mataifa hayo ni kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika ambako vitendo vya rushwa vimekithiri na kuifanya baadhi ya misaada kutowafikia walengwa.

No comments:
Post a Comment