"SIMTAKI HAKIMU HUYU HANITENDEI HAKI"
Mchungaji Christopher Mtikila amewasilisha ombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana akitaka hakimu anayesikiliza kesi ya kutoa lugha ya uchochezi na kumkashifu Rais Jakaya Kikwete, Bw. Genivitus Dudu kwa madai kuwa hawezi kutenda haki na hamuamini.
Mchungaji Mtikila aliwasilisha hati hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Bw.Walialwande Lema jana kabla za kesi kuahirishwa mpaka June 30, ikiwa ni mara ya pili kuomba abadililishiwe hakimu.
Kwa mujibu wa barua hiyo ilizosainiwa naye na nakala zake kupelekwa kwa Mwendesha Mashitaka wa Serikali na Kampuni ya wakili wake ya Mpoki & Associeties, Mtikila anadai hakimu hatendi haki katika shauri hilo.
Sababu nyingine zilizotolewa katika barua hiyo ni pamoja na kunyimwa muda wa siku mbili kupitia hati za majadiliano na wakili wake na kupewa dakika tano za majadiliano kabla ya Mahakama kuendelea.
Pia Bw. Dudu alitupilia mbali ombi la Wakili wa Mtikila la kutaka mkanda wa video usioneshwe Mahakamani kama ushahidi kutokana na kutojua kilichokuwepo ndani.
Aidha Hakimu huyo amedaiwa kuendesha kesi hizo kwa maslahi ya upande wa mashitaka, kwakua mawakili wake waliiomba kuhamishia kesi hiyo Mahakama kuu kwa ajili ya mapitio na kunyimwa wakiwa chumba cha mawakili.
Iliongeza kuwa kutokana na uadua wa kisiasa fili la kesi hizo liliombwa na na Wakili wake ili ipielekwe katika Mahakama kuu ili haki itendeke na kunyimwa kwa madai kuwa kuwa lipo kwa Bw.Dudu.
Februari 1 mwka huu Bw.Mtikila aliwasilisha ombi Mahakamani hapo akitaka hakimu anayesikiliza kesi yake, Hakimu Mkazi Mkuu, Bw. Walialwande Lema ajitoe kuendesha kesi yake kwa madai kuwa hamuamini.
Bw.Mtikila alimuomba Hakimu Lema kujitoa katika mwenendo wa kesi yake kwa sababu alionyesha kuwa na kisirani na ukatili dhidi yake na kumfokea ovyo kwa sababu ambazo akidai kuwa anazo moyoni mwake.
Bw.Mtikila anayekabiliwa na kesi ya kutoa lugha ya uchochezi na kumkashifu Rais Jakaya Kikwete, inayosikilizwa Bw.Dudu, aliwasilisha barua ya kuomba hakimu huyo ajitoe jana.
Alidai tukio la kwanza ni pale alipochelewa mahakamani, mara baada ya kuitwa kwa kesi yake na kuamriwa akamatwe na kufikishwa mbele ya hakimu huyo.
Alidai alielezea sababu ya kuchelewa ilitokana na suruali yake kuchanika akiwa njiani kwenda mahakamani, hivyo kulazimika kurejea nyumbani kuibadili na kuwa hata mdhamini wake hakuwepo.
Alidai mbali na tukio hilo Januari 11, mwaka huu, alipofika mahakamani akiwa amechelewa kutokana na maumivu ya mguu aliogongwa na nyoka nchini Zimbabwe, lakini hakimu alimfutia dhamana na kumrejesha gerezani.
Awali, wakili wa Serikali Bi.Monica Mbogo alidai mbele ya Hakimu Bw.Bw. Walialwande Lema kuwa mshtakiwa ambaye ni Mtanzania Mkazi wa Ilala jijini Dar es salaam alitenda kosa hilo Oktoba 21 mwaka 2007.
mwisho

No comments:
Post a Comment