BAADHI ya wananchi jijini Dar es Salaam wameiomba Serikali, kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kutowachukulia hatua wanasiasa wanaowania majimbo mbalimbali na kutoa msaada.
Wamedai kuwa wanasiasa hao wamekuwa wakitoa misaada katika kipindi na mara wachaguliwapo huwa hawaonekani tena.
Mmoja wa wananchi hao Juma Nasibu Mjonge amesema, kutokana na viongozi kuwa wajanja wajanja mara wanapopata madaraka kipindi hiki ni kizuri wa wananchi kwa kupata misaada hiyo.
Amedai kuwa asilimia kubwa ya viongozi wanaochaguliwa huyasahau majimbo yao na wengie huishia kujenga nyumba za kifahali.
“Unajua TAKUKURU wakiwakamata hawa ni kama wanatuharibia sisi kwani hawa viongozi sasa hivi wanakuja na ndo muda mzuri,” amesema Juma.
Mkazi mwingine Salehe Ibrahim yeye amemuomba Rais Jakaya Kikwete awaruhusu viongozi kupitia TAKURURU viongozi hao waruhusiwe kutoa misaada kwa wananchi.
“Kweli kuna sheria inayokata wagombea wasitoe misaada lakini sisi tunamwomba Rais Kikwete awatuhusu hawa wagombe ili na sisi tupate misaada hiyo,” amedai mkazi huyo.
.

No comments:
Post a Comment