header

nmb

nmb

Thursday, June 17, 2010

WACHAKACHUAJI MAFUTA MTATUMALIZA LAKINI SASA KUKIONA!!


BAADHI ya wakazi jijini Dar es Salaam wamewaomba wafanyabiashara wenye tabia ya kuchanganya mafuta ya taa na maji ili kupata faida kubwa kuacha mara moja ili kupunguza adha kwa watumiaji.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamesema kuna tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kujichukulia uamuzi wa kutaka kujinufaisha kwa kuongeza maji katika mafuta ya taa hali ambayo imekuwa ikiwapa usumbufu watumiaji
Mary John mkazi wa Temeke amesema amejikuta katika wakati mgumu kwa kulazimika kumwaga mafuta mara kwa mara kutokana na hali hiyo.
Amesema awali alikuwa hajagundyua tatizo hilo na kulazimika kumwaga mafuta katika jiko lake la mafuta na kununua mengine bila mafanikio.
Amesema tabia hii imekuwa ikiwalazimu kujikuta wakiingia gharama kwa kununua tambi zingine kwa ajili ya kuweka kwenye jiko hali ambayo imekuwa ikiwapa usumbufu mkubwa.
Naye Sada Mussa amesema amejikuta akichelewa kuandaa chakula chake kutokana na jiko kutokuwaka.
Amesema hali hiyo imemuweka katika wakati mgumu na kulazimika kutumia mkaa hata pale anapotaka kuandaa chakula cha haraka.
Wameiomba serikali kupitia mmlaka zinazohusika kuliingilia suala hili nna kuwachukulia hatua wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kuwapa adhabu kali kisheria.


Dar Leo ya Leo

No comments:

Post a Comment