header

nmb

nmb

Tuesday, June 29, 2010

MGONJWA AUWA MGONJWA MWENZAKE WODINI MOSHI!!



WATU watatu wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti mkoani Kilimanjaro likiwemo la ajali ya pikipiki iliyosababisha vifo vya watu wawili.
Akitoa taarifa ya matukio hayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Lucas Ng’hoboko alisema tukio la kwanza lilitokea Juni 24 mwaka huu, saa mbili na Robo usiku na kuhusisha Gari Na.T 992 APN Isuzu Tipper na Pikipiki Na T 859 BFV aina ya Sunflag.
Alisema mazingira ya tukio hilo Bw. Ng’hoboko alisema gari hilo lililokuwa likiendeshwa na Bw. Anasael Swai (35) Mkazi wa Boma la Ng’ombe wilayani Hai liligongana na Pikipiki na kusababisha vifo vya wapanda pikipiki wawili papo hapo.
Bw Ng'hoboko aliwataja waliofariki kuwa ni Dereva wa pikipiki hiyo ambaye ni Daraja Costantine Shirima (33) Mkazi wa Holili wilayani Rombo na Isack Mtui (29) mkazi wa Himo wilayani Moshi ambaye alikuwa abiria wa Pikipiki hiyo.
Kwa mujibu wa kamanda chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari na kwamba dereva anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi kuhusu ajali hiyo na miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi.
Katika tukio la pili mgonjwa akili katika hospitali Kilimanjaro Mawenzi amemuua mgonjwa mwenzake wa akili wakati wakiwa wodini.
Akielezea tukio hilo Bw Ng' hoboko alisema, tukio hilo lilitokea Jun 24 mwaka huu wakati wa mchana hospitali hapo ambapo walikuwa wamelazwa wagonjwa hao.
Kwa mujibu wa kamanda Ng’hoboko taarifa ziliripotiwa na uongozi wa Hospitali hiyo kwamba wamebaini kuwa katika wodi ya wagonjwa wa akili Bw.Hamisi John (24)ambaye ni mgonjwa wa akili aliyekuwa amelazwa katika wodi hiyo aliua usiku na mgonjwa mwenzake wa akili Bw. Ramadhani Joho (24).
Aidha kamanda alisema kuwa uchunguzi unaonyesha kuwa marehemu na mtuhumiwa walilazwa hospitalini hapo kwa nyakati tofauti katika wodi ya wagonjwa wa akili.Imeandikwa na Frola Temba wa Mosho majira

No comments:

Post a Comment