WAKATI leo ni hitimisho ya usajili wa namba za simu za mikononi, baadhi ya vituo vya kusajili wamelazimika kukesha ili kusajili laini kutokana na mrundikano wa wateja.
Mbali ya kuwepo kwa hali hiyo hofu na mashaka vimewakumba baadhi ya wateja kutokana na kupata ujumbe kuwa laini zao hazijasajiliwa wakati tayari wamezisajili.
Kutokana na hofu hiyo baadhi ya wateja wamelazika kukesha kwenye vituo ili kujiandikisha tena.
Hali hiyo imejitokeza katika Uwanja wa Biafra Kinondoni ambapo uwanja huo hivi sasa unatumika kwa ajili ya kuangalia michuano ya Kombe la Dunia.
Wakati wapenzi hao wakiendelea kuangalia ligi hiyo gazeti hili lilishuhudia wakala wa kampuni za Zain na TIGO walionekana wakiendelea kusajili laini za wateja.
Msururu wa wateja hao ulionekana kuwa mkubwa na kushangaza baadhi ya watu kuwa wateja hao hawajahi kusikia taarifa za usajili wa laini.
"Tunaomba kampuni za simu zisitufungie laini kwani sisi tulishasajili lakini tumelazimika kurudi tena baada ya kutumiwa ujumbe kuwa laini zetu hazijasajiliwa, " alisikika akidai mteja mmoja.
Baadhi ya wateja waliozungumza na gazeti hili wameziomba kampuni za simu kuwa makini na usajili wa laini ili kuwaondolea usumbufu na hata kuweza kupoteza wateja.
"Kuna wateja wengine wameamua kuacha kusajili tena na kuamua kuondoka saa 5 usiku kwani wakituma ujumbe katika namba 106 hupata majibu kuwa laini zao hazijasajiliwa na kupatwa na hofu, " amedai mteja mwingine.,
Pia baadhi ya wateja wengine wamedai kuwa majina yao yamekosewa jambo ambalo limewapa hofu na kulazimika kutuma ujumbe ambao hauna majibu.
Katika uchunguzi wa gazeti hili baadhi ya wateja kutoka maeneo ya Mbagala wamelazimika kulipa fedha kuanzia sh. 1000 hadi 2,000 kwa kununua watu waliosimama mbele na kuweza kusajili laini zao.
Hata hivyo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TRCA) imesema haitaongeza tena muda wa kusajili namba za simu na leo usiku saa 6 itazifungia laini zote zisizosajiliwa.
Aidha kampuni za simu zimeomba kuongezwa muda zaidi kwa kuhofia kupoteza wateja wao.

Dar Leo ya leo
No comments:
Post a Comment