HAKIMU mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Joyce Minde, amesema ametupilia mbali ombi la kupitia upya kesi ya madai inayomkabili Mchungaji Christopher Mtikila badala yake amemwagiza afike mahakamani ili ajieleze kwanini asihukumiwe kwa kesi ya madai inayomkabili.
Hakimu Minde aliamua kutoa uamuzi huo baada ya kuona Mtikila hakufika mahakamani hapo bila kutoa taarifa yoyote ya kutofika huku akiwa anafahamu kuwa anahitajiwa mahakamani hapo.
Minde amesema ombi la kupitiwa upya kesi ya Mtikila imechelewa kuletwa mahakamani hapo kwa hiyo anatakiwa alipe fidia kwa mdai kama gharama za usumbufu ambazo amemsababishia mdai ambaye ni Paskazia Matete.
Amesema Juni 14, mwaka huu, Mtikila anatakiwa afike mahakamani ili hukumu iweze kutolewa dhidi yake na mwenzake Mariamu Issa.
“Juni 14, mwaka huu, nitatoa hukumu dhidi ya Mtikila na Mariamu na pia nitamwambia Mtikila ajieleze kwanini asifungwe kifungo cha madai kwanza kisha masuala mengine yafuate, amesema Minde.
Awali Mchungaji Mtikila na mwenzake walifikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na kesi ya madai ya sh. milioni 9 ambazo wanadaiwa na Paskazia Matete.esi hiyo ilikuwa kwa hakimu Kibona na baadaye ilihamishiwa kwa hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo kwa ajili ya kutoa uamuzi lakini kesi hiyo imeahirishwa mara tatu kutolewa hukumu kwa sababu mbalimbali zinazodaiwa na Mtikila.
Wakati huo huo, kesi nyingine inayomkabili Mchungaji Mtikila katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kumkashifu Rais Jakaya Kikwete imeunguruma leo katika mahakama hiyo.
Katika kesi hiyo leo asubuhi wakili wa Mtikila aliiomba mahakama isianze kusikiliza kesi hiyo na kuomba apewe muda wa siku mbili ili kupitia vielelezo.
Hata hivyo Hakimu Genivitus Dudu alikataa ombi hilo na kumpa muda wa saa moja wakili huyo ili kupitia vielelezo hivyo.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na Ponsiano Lucos umesema wapo tayari kuanza kusikilizwa ambapo leo wamemleta shahidi mmoja.
Awali ilidaiwa kuwa kuwa Oktoba 21, mwaka huu akiwa Ilala, Dar es Salaam alitoa maneno ya uchochezi yenye nia ya dharau ambayo yalilenga kusababisha mtafaruku katika Serikali ya Tanzania kutokana na kudai kuwa Rais Jakaya Kikwete.
Hadi tunakwenda mitamboni kesi hiyo ilikuwa bado ikiendelea kusikilizwa.

No comments:
Post a Comment