header

nmb

nmb

Tuesday, June 1, 2010

88.4 WATIMIZA MWAKA MMOJA TANGU WAINGIA MJENGONI MAIKOCHEN!!

Mkurugenzi mkuu wa Redio hiyo Bw. Joseph Kusaga(katikati) akiwa na wadau

Kituo maarufu cha redio nchini, Clouds 88.4 FM, leo kimetimiza mwaka mmoja tangu kilipohamia katika jengo lake eneo la Mikocheni B karibu na Daraja la Mlalakuwa, pembeni mwa barabara inayoelekea kilipo kiwanda cha Coca Cola jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kuhamia jengo hilo, Clouds FM ilifanya shughuli zake kwa zaidi ya miaka kumi katika jengo la Kitega Uchumi lililopo Barabara ya Sokoine.

Mhariri na timu nzima ya pr Promotion na prblog inaupongeza uongozi wote wa Clouds Entertainment, pamoja na wafanyakazi wa Clouds FM, hususani kipindi cha Jahazi na watangazaji wake Gardner Habash, Ephraim Mafuru na muandaaji kipindi hicho Semalengo.

No comments:

Post a Comment