MAHAKAMA ya Wilaya Temeke jana ilizizima kwa vilio na majonzi yaliyochanganyikana na furaha baada ya mahakama hiyo kumhukumu mshtakiwa Halfani Abdallah (28) kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wake kiume mwenye umri wa miaka sita.
Umati wa watu, wakiwamo majirani, ndugu na jamaa waliokuwa wakifuatilia kesi hiyo, ulifurika katika mahakama hiyo kusikiliza hukumu ya mshtakiwa huyo iliyotolewa na hakimu wa mahakama hiyo, Rukia Kalili
Kesi hiyo ambayo ilivuta hisia za watu wengi na hasa majirani wanaoishi na mshtakiwa kutokana na kitendo alaichokuwa akikifanya mshtakiwa.
Upande wa mashtaka ulidai kuwa mshtakiwa huyo, ambaye ni mkazi wa Kigugumo, Kigamboni, amekuwa akimfanyia mwanawe vitendo viovu na kumsababishia afya yake kuzorota.
Ilidaiwa kuwa awali mshtakiwa huyo alikuwa na mke ambaye aliondoka kutokana na kumwingilia kinyume cha maumbile.
Ilidaiwa kuwa kutokana na vitendo hivyo mkewe hakuweza kuhimili na kuamua kurudi kwa wazazi wake ambapo kwa aibu mshtakiwa huyo aliamua kuhama kutoka Ubungo kwenda Kigamboni.
Baada ya kuhama mshtakiwa huyo aliamua kuishi na mtoto wake wa kiume lakini kadri siku zilivyokuwa zikienda afya ya mtoto huyo ilikuwa ikizorota.
Imedaiwa kuwa kila inapofika kati ya saa 10 na 11 alfajiri mtoto huyo alikuwa akipiga kelele, jambo lililowapa hofu majirani na kuamua kuweka mtego.
Imedai kuwa katika mtego huo majirani hao walifanikiwa kugundua kitendo alichokuwa akifanya mshtakiwa kwa mtoto wake baada ya kuchungulia dirishani.
Baada ya kubaini kitendo hicho majirani walitoa taarifa kwa uongozi husika ndipo mshtakiwa aliponasa kwenye mtego.
Aidha mtoto huyo, katika utetezi wake mahakamani hapo, alidai kuwa ni kweli baba yake amekuwa akimwingilia kinyume cha maumbile kwa kumpaka mafuta.
Mtoto huyo alimweleza hakimu namna ambavyo sehemu zake za siri zilivyo za baba yake kuwa ni kubwa na amekuwa akimwingilia sehemu ya haja kubwa kila siku.
Mtoto huyo alidai kuwa kabla ya baba yake kumfanyia kitendo hicho kwanza humpaka mafuta licha ya kulia lakini baba huyo huendelea kumfanyia unyama huo.
Baada ya hakimu kumaliza kusoma mwenendo wa kesi hiyo, baadhi ya watu waliokuwa wakifuatilia walianza kulia jambo lililomsababisha mshtakiwa huyo naye kuanza kutokwa machozi.
Kabla ya kusoma hukumu hiyo, hakimu huyo alimpa nafasi mshtakiwa ajitete ambapo aliiomba mahakama isimpe adhabu kali kwani yeye ni mgonjwa wa fangasi na pia mishipa yake imevimba.
Baada ya kutoa ombi hilo, hakimu alitoa hukumu kuwa kutokana na kosa hilo mahakama katika utetezi wa walalamikaji umethibtisha kuwa mshtakiwa alikuwa akifanya kitendo hicho hivyo uliamuru mshtakiwa kupewa adhabu ya kifungo cha maisha jela.
Kutokana na hukumu hiyo baadhi ya watu waliofika mahakamani hapo walishangilia na wengine kumsikitikia kwa adhabu aliyopewa.
Awali ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo Mei 15, 2009, alimwingilia kinyume cha maumbile mtoto wake na kumsababishia afya yake kuzorota.
Stera Alon wa Gazeti la Dar leo
No comments:
Post a Comment