header

nmb

nmb

Wednesday, June 2, 2010

NGOZI YA BINADAM NI PESA MKOANI MBEYA, BIBI KIZEE ACHUNWA!!

HOFU na mashaka vimewakumba tena baadhi ya wananchi mkoani Mbeya baada ya mwanamke mmoja kuchinjwa na kutenganishwa kichwa na kiwiliwili na kisha kuchunwa ngozi usoni.
Mwanamke huyo alikutwa kwenye pori lililopo katika kijiji cha Kalalo wilayani Rungwe ambapo imedaiwa kuwa alikuwa akitoka matembezini.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu wamedai kuwa mwanamke huyo alikutwa kwenye eneo la pori ambalo hakuna watu wanaoishi karibnu na pori hilo.
Kufuatia kwa tukio hilo baadhi ya wananchi mkoani humo wameingia na hofu kuwa huenda matukio ya mauaji na uchunaji ngozi yakaanza kurejea tena.
"Tunawasiwasi kuanza kwa matukio ya uchunaji ngozi ambayo yalitusababishia hofu kubwa, " alidai mkazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Noel Mwakifulefule.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Advocate Nyombi amethibisha kuwepo kwa tukio hilo hilo ambapo amesema kuwa maiti ya mwanamke huyo ilikutwa Mei 27 saa 8 mchana katika kijiji cha Kalalo wilayani Rungwe.
Amesema kuwa mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Alice Kosia (70) ambaye alikuwa akitokea kilabuni.
Kamanda amesema kuwa mwili wa marehemu ulikutwa na majeraha mbalimbali ambapo kichwa kilikuwa kimetenganishwa na kiwiliwili.
"Hatujaona kama ngozi ilikuwa imechunwa isipokuwa tuliikuta maiti hiyo ikiwa imetenganishwa kichwa na kiwiliwili katika pori hilo, " amesema kamanda.
Amesema kuwa katika uchunguzi wa awali imebainika kuwa marehemu alikuwa na ugomvi wa mashamba na ndugu zake.
Amesema jeshi la polisi linawashikilia ndugu sita kuhusiana na tukio hilo kwa ajili ya mahojiano zaidi.

No comments:

Post a Comment