BAADA ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuomba kupandisha gharama za umeme, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imewataka wananchi wenye pingamizi juu ya ombi hilo kujiandikisha ili kutoa maoni yao kabla ya Julai 14 mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Haruna Masebu imeelezwa kuwa wananchi watakaojiandikishwa watapewa fursa ya kuwasilisha maoni yao katika mikutano husika.
Masebu amesema kuwa kulingana na kifungu cha sheria za nchi, EWURA imeanza mchakato wa kukusanya maoni ya wadai kuhusu uhalali wa ombi la TANESCO la kuidhinishwa ongezeko la bei za huduma ya umeme kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Januria kosi 2011.
Amesema kuwa TANESCO wameomba bei za huduma ya umeme ziongezeke kwa asilimia 34.6 kwa mwaka 2011 na asilimia 13.8 kwa mwaka 2012 na asilimia 13.9 kwa mwaka 3013 hivyo wananchi watatakiwa kutoa maoni kwenye mikutano itakayofanyika katika mikoa na tarehe itakayopangwa.
Amesema kuwa wananchi wote wanaotaka kuweka pingamizi kuhusiana na ombi hilo wanatakiwa kujiandikisha EWURA kabla ya saa 11Julai 14 mwaka huu.
"Wale watakaojiandikisha watapata fursa ya kutoa maoni yao papo kwa hapo katika mikutano ndani ya kipindi cha wiki mbili na wasiojiandikisha pia watapewa fursa ya kutoa maoni yao papo kwa hapo, " amesema Masebu.
Hata hivyo baadhi ya wananchi waliohojiwa na gazeti hili wamedai kuwa kutokana na gharama hizo kuongeza pia kunaweza kusababisha kuongeza kwa gharama za maisha.
Wamedai kuwa endapo TANESCO itapandisha bei ya umeme basi kuna uwezekano wa bidhaa zingine kupanda bei na kusababisha maisha kwa walalahoi kuzidi kuwa magumu.
Rajabu Hamisi mkazi wa Kinondoni B amedai kuwa kabla ya kupandishwa kwa bei ni vizuri kwanza TANESCO wakaboresha miundombinu ili kuepuka kero kwa wateja.
Amedai kuwa kero ya kuwepo kwa umeme mdogo katika maeneo mengi jiji imekuwa ni ya muda mrefu lakini TANESCO imeshindwa kuchukua hatua.
Mkazi mwingine wa Temeke, Taliki Issa amedai kuwa mbali ya kuwepo kwa kero ya umeme mdogo pia kumekuwa na kero ya matatizo ya LUKU pindi mteja anapotaka kuingiza umeme.
"Kuna wakati ukinunua umeme wa LUKU na ukianza kuingiza namba zilizo kwenye karatasi zinakataa kuingia na kutakiwa kwenda Makao Makuu ili kuboreshewa huduma hivyo na hii imekuwa kero kwa watu wengi, " amedai mkazi huyo.

No comments:
Post a Comment