MKUU wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga amesema kuwa wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani ambao mabasi yao yatabainika kutofungwa mikanda watafikishwa mahakamani.
Akizungumza na Dar Leo leo asubuhi, amesema kuwa oparesheni kali ya kuyanasa mabasi hayo inatarajia kuanza kesho kutwa.
"Julai Mosi tunatarajia kuanza operesheni ya kuyanasa mabasi yasiyofunga mikanda kwani ni muda mrefu lilitolewa agizo kwa wamiliki hao kuhakikisha kuwa mabasi yao wanayafunga mikanda, " amesema.
Amesema kuwa agizo hilo liliwataka wamiliki wa mabasi kuhakikisha kuwa wanafunga mikanda mabasi yao ili kuweza kuwanusuru Watanzania pindi ajali zinapotokea.
Amesema kuwa kwa mujibu wa kanuni ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Majini na Nchikavu (SUMATRA) ya mwaka 2007 kila basi liendalo mwendo mrefu linatakiwa kufunga mikanda kwa ajili ya abiria.
"Hatutomkamata dereva wa kondakta bali tutawakamata wamiliki wa mabasi kwa kosa la kutofunga mikanda kwani ndio wenye jukumu hilo, " amesema Mpinga.
Mpinga amesema kuwa pia utaratibu kwa magari yaendayo Kongowe, Bagamoyo, Kibaha, Msata ambayo magari mengi ni aina ya Coaster pia yatatakiwa kufunga mikanda.
"Tumeanza na magari ya mwendo mrefu na kisha baada ya tutafuatia magari ya masafa mafupi nia ni kuboresha huduma za usafiri, " amesema. Aidha ameongeza kuwa kwa upande wa magari aina ya daladala bado mkakati unaendelea namna ya kuweza kufungwa kwa mikanda.

No comments:
Post a Comment