JESHI la Polisi nchini Afrika Kusini limesema kuwa mwanamume raia wa nchi hiyo ameuawa kwa kupigwa na mkewe na wanaye baada ya kuibuka ugomvi wa kugombea kuangalia vipindi katika televisheni.
Kwa mujibu wa taarifa za Polisi hao, David Makoeya (61), mkazi wa kijiji kidogo cha Makweya kilichopo katika Jimbo la Limpopo aliuawa na mkewe akishirikiana na wanawe wawili Jumapili iliyopita wakati wakigombea ‘rimoti’ baada ya baba kutaka kuangalia mechi kati ya Ujerumani na Australia katika michuano ya fainali za Kombe la Dunia wakati wengine wakitaka kuangalia tamasha la muziki wa injili.
“Alisema hapana nataka kuangalia mpira,” msemaji wa Polisi, Mothemane Malefo, alisema jana.
“Na hapo ndipo ubishi ulipoanza na kuanza kumshambulia,” aliongeza.
Malefo alisema baada ya ubishi huo Makoeya aliamka na kutaka kubadilisha chaneli kwa kutumia mkono baada ya kunyimwa rimoti na hapo ndipo alipoanza kushambuliwa na mkewe, Francina 68 na watoto wake Collin (36) na mdogo wake Lebogang (23)
Hata hivyo, Malefo alisema hawana uhakika kitu walichokitumia kumuua Makoeya.

No comments:
Post a Comment