header

nmb

nmb

Friday, June 18, 2010

WACHINA NDANI KWA KUTILILISHA MAJI TAKA JIJINI!!


WASHITAKIWA Funi Zheng (24) na Li Jin (40), raia wa China, wamefikishwa katika Mahakama ya Jiji kujibu mashitaka ya kutiririsha maji yenye kinyesi.

Washitakiwa kwa pamoja wamesomewa mashitaka yao na mwendesha mashitaka wa polisi Jonh Kijumbe mbele ya Hakimu Agustina Mmbando.

Imedaiwa kuwa Juni 14, mwaka huu, asubuhi, Kurasini washitakiwa kwa pamoja walikamatwa na Afisa Afya wa Manispaa ya Temeke Asia Mohamed wakiwa wanatiririsha maji yaliochanganyikana na kinyesi huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Washitakiwa wamekiri kutenda kosa na mahakama imewaamuru kulipa faini ya sh. 100,000 kila mmoja.

Katika kesi nyingine, mshitakiwa Mihayo Rashid (30) mkazi wa Manzese amefikishwa katika mahakama hiyo kujibu shitaka la kutupa taka ovyo.

Mshitakiwa amesomewa shitaka lake na mwendesha mashitaka wa polisi Jonh Kijumbe mbele ya hakimu Agustina Mmbando wa Mahakama ya Jiji.

Imedaiwa kuwa Juni 14, mwaka huu,saa 4 asubuhi, Manzese Darajani mshitakiwa alitupa taka katika sehemu isiyoruhusiwa na kukamatwa na Afisa Afya wa Manispaa ya Kinondoni Joyce Mtuli.

Mshitakiwa amekana mashitaka na kesi yake itatajwa tena Juni 25, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment