header

nmb

nmb

Tuesday, May 4, 2010

UJIO WA WAGENI DAR KOVA APANIA KUZIBA RIZIKI ZA VYANGUDOA!!
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleiman Kova, amesema jeshi lake limeanza rasmi kuthibiti madada poa (changudoa) ambao wamejikusanya karibu na hoteli kubwa za Dar es Salaam ambazo wageni wamefikia kwa lengo la kuuza miili yao.

Akizungumza leo katika kipindi maalumu cha Jambo Tanzania kinachorushwa kila siku na Televisheni ya Taifa (TBC1), amesema juzi walipata taarifa kutoka kwa watu mbalimbali na usiku wa kuamkia leo wamefanya msako wa kuwakamata.

Amesema dada hao wameongezeka katika hoteli zote kubwa na kuanza kuzunguka zunguka karibu na geti za hoteli hizo wakiwa na mavazi yasiyofaa wakitaka kujipatia riziki kupitia wageni wanaohudhuria Mkutano wa Kiuchumi Duniani (WEF).

Kova amesema dada hao ambao wamebuni njia mbadala ya kujikusanya kwenye miti na sehemu za giza kwa kupeana mikakati kabambe ya kujinufaisha kutokana na wageni, mara tu wanapooana gari mmoja hujitokeza kwa madaha akijipitisha karibu nalo.

Amesema atahakikisha kuwa akina dada hao wataondolewa kwa njia yoyote ile na kwamba ameweka ulinzi saa 24 kuzunguka hoteli zote mpaka mkutano huo utakapomalizika.

Kova amesema Tanzania inajulikana kuwa nchi ya amani na utulivu, hivyo ujio wa wageni nchini unatakiwa kuondoka na sifa ile ile na siyo kupata picha mbaya kutoka kwa dada wetu.

Amesema kawaida ya madada hao ni wizi wa vitu vya wageni zikiwapo fedha, kamera, nguo na vitu vingine mbalimbali.

Ikiwa wataruhusiwa kuwa karibu na wageni hao matukio ya uhalifu na wizi yataongezeka na kusababisha kuchafuliwa kwa sifa tulinayo.

Kova amesema hivi sasa hoteli zote kubwa zimejaa wageni ambao tayari jeshi la polisi limejithatiti kuwahakikishia usalama wao hadi watakapomaliza mkutano huo.

Akizungumzia usalama kwa jijila Dar es Salaam amesema ulinzi uliowekwa haujawahi kutokea na ni tofauti na ule uliowekwa wakati aliyekuwa Rais wa Marekani, George Bush, alipotembelea Tanzania.

Amesema pikipiki, farasi, helikopta na gari za polisi na makacheroa wamesambazwa sehemu zote za jiji pia kuna kamera zimefungwa kunakili matukio.

“Kuingia katikati ya jiji na kufanya uhalifu na kufanikiwa kutoroka na mali ya mtu ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa, labda matukio kama hayo yafanyike nje ya jiji,” amesema Kova.

Kova amewaomba wanachi na wamiliki wa hoteli kutoa ushirikiano wa karibu kwa jeshi la polisi wanapoona dalili zisizo za kawaida, vile vile kuhifadhi mali zozote za wageni mara inapotokea bahati mbaya kujisahau.By.Dar leo Tanzania

No comments:

Post a Comment