header

nmb

nmb

Tuesday, May 4, 2010

MAJAMBAZI WA MKURUGENZI WA NSSF, BW.DAU KIZIMBANI!!


Mkurugenzi wa Nssf Bw. Dau

WASHITAKIWA watano—Khatibu Kaninki (45), Patrick John (44), Paulo Shirima (42), Rajabu Dinguge (45) na Salehe Kikunde (35)—wakazi wa jijini Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu mashitaka ya unyang'anyi wa kutumia nguvu nyumbani kwa Mkurugenzi wa NSSF Ramadhani Dau.

Imedaiwa Mahakamani hapo kuwa Aprili 17, mwaka huu, washitakiwa waliiba nyumbani kwa mlalamikaji vitu mbalimbali zikiwamo nyaraka mbalimbali, bastola, risasi, boksi la fedha, saa za ukutani—vyote vikiwa na thamani ya sh. 15,000,000.

Mbele ya Hakimu Frednand Kiwonde imedaiwa na Mwendesha Mashitaka Inspekta wa Polisi Edwin Boniphace.

Washitakiwa wamekana mashitaka na kesi hiyo itatajwa tena Mei 17, mwaka huu.

Pia, God Msishiri (31), mkazi wa Kawe amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu mashitaka ya wizi wa kutumia silaha.

Imedaiwa Mahakamani hapo kuwa Aprili 19, mwaka huu, mshitakiwa aliiba bastola, kompyuta, na simu ya mkononi ambazo thamani yake ilikuwa ni sh. 4,000,000 mali ya mlalamikaji Russ Doering.

Mbele ya Hakimu Suzan Kihawa imedaiwa na Mwendesha Mashitaka Inspekta wa Polisi Nassoro Sisiwaya kuwa, mshitakiwa aliiba vitu hivyo.

Mshitakiwa amekana mashitaka na kesi hiyo itatajwa tena Mei 17, mwaka huu. By.Dar Leo

No comments:

Post a Comment