header

nmb

nmb

Tuesday, May 4, 2010

KWA BITI HILI TUCTA WAUFYATA!, WADAI KUJIBU MAPIGO LEO!!

Rais JK Kikwete; Hakuna mgomo hapa

Viongozi wa TUCTA; Hii ni nchi yetu ya kidemokrasia

Rais Kikwete amewashukia wafanyakazi hao, hasa viongozi wa Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi (TUCTA) kuwa wamekuwa si wakweli, na wamekuwa wakibadilika kila kukicha na kukana mambo ambayo waliyokubaliana na kutia saini.

Ingawa viongozi hao walishasema kuwa walichoafikiana na serikali ni kutokukubaliana, Rais Kikwete alisisitiza kuwa viongozi hao walishafikia makubaliano, wakatia saini juu ya viwango vya mishahara, lakini baadaye wakabadilika.

"Viongozi wa TUCTA ni waongo si wakweli, wanachofanya ni kuwadanganya wafanyakazi washiriki kwenye mgomo ili watekeleze malengo ya waliowatuma kushinikiza mgomo huo," alisema Rais Kikwete.
Aliongeza kuwa mgomo ulioitishwa na TUCTA, si halali kwani mazungumzo juu ya madai yao, yanaendelea baada ya serikali kuwaeleza ukweli viongozi hao kuwa, kima cha chini cha mshahara walichopendekeza bado ni kikubwa na hakitekelezeki.

"Kama kuna mfanyakazi wa serikali ambaye atashiriki mgomo huo, hatutasita kumuwajibisha, hata yule ambaye atakwenda kazini lakini asifanye kazi, naye atawajibishwa bila kuoneana huruma," alisisitiza Rais Kikwete na kuongeza kuwa, yeye ndio mwajiri mkuu , hivyo wafanyakazi wanapaswa kumsikiliza na sio viongozi wa TUCTA.

"Yule dereva teksi atawajibishwa na mwenye gari, na yule dereva wa daladala atawajibishwa na tajiri wake, lakini kwa serikali mimi ndiye mwajiri, nitahakikisha wanawajibika," alisema.
Alisema kuwa madai ya TUCTA ya kulipwa kiasi hicho cha mshahara ni sawa na kuwadhulumu Watanzania ambao si wafanyakazi.

Aidha, alisema Serikali ina kila sababu ya kuwahoji viongozi wa TUCTA kuhusu dhamira yao ya kusisitiza mgomo kama wana nia njema au kuna jambo jingine.

Aliongeza kuwa kiwango hicho cha fedha ni sawa na kuwa na bajeti ya zaidi ya sh. trilioni 6 kwa mishahara pekee, wakati mapato ya serikali ni sh. trilioni 5, hivyo mahitaji hayo ya wafanyakazi ni zaidi kuliko mapato.

Sambamba na hayo Rais Kikwete hakusita kuonesha hisia zake katika siasa kuhusiana na vitisho vya TUCTA kutowapigia viongozi wanaowadai kuwa hawatekelezi matakwa yao, ambapo alisema kuwa hata kama hawatapiga kura, basi wasimpigie kwani zitapatikana kwa wengine.
"Kama hamtataka kunipigia kura acheni kwani tutazipata kwa wengine ambao wanataka kudhulumiwa na wafanyakazi," alisema kwa msisitizo.

Aidha aliwataka viongozi kusema ukweli daima hata kama ukwelihuo utawaumiza wale waliowaomba wakasikilize au kupeleka hoja zao.

Mkutano huo ulianza saa 11:05 na kumalizika saa 12:45 ambapo ulionesha kuvuta hisia za wazee ambapo baadaye viwanja hivyo viligeuka kuwa wa shamrashamra za kumpongeza rais kwa tamko lake

No comments:

Post a Comment