header

nmb

nmb

Tuesday, May 4, 2010

BURUNDI NAO WAANZA TENA MAUAJI YA ALBINO, WAWACHINJA WAWILI KAMA KUKU NA KUUWA WAZAZI WAO..!!

Watoto wenywe ulemavu wa ngozi wakiwa katika hofu kubwa pichani nchini Burundi.
kwa sasa hawana amani tena

Albino wa Bongo anayeteseka kwa kukatwa mkono


Mauaji ya Albino bado yanaendelea Burundi.Watu waliokuwa wamejihami kwa mapanga,Bunduki na Mabom ya kutupwa kwa mkono wamemuua mwanamke Albino na mtoto wake wa miaka minne ambao ni albino ikiwemo na Baba mwenye nyum,ba ambaye si albino ambaye alikuwa akiwahami wanawe nchini Burundi usiku wa kuamkia leo.

Inaarifiwa kuwa maiti za wawili hao ilikatwakatwa vibaya katika mkoa wa Cankuzo, unaopakana na Tanzania.
Mwenyekiti wa chama cha maalbino nchini humo, Kassim Kazungu, ameelezea BBC kuwa anashuku wauaji walitoroka gerezani na walikuwa wamehukumiwa kwa makosa ya kuwashambulia maalbino.

Aliongeza kuwa shambulio kama hilo halijashuhudiwa Burundi katika kipindi cha mwaka mmoja.Baadhi ya watu wanaamini kuwa viungo vya mwili wa albino vinaweza kuwatajirisha. Katika tukio hilo la kutisha Majambazi hao waliondoka na Titi la mama Upande mmoja wa kichwa na viganja vya mikono. Polisi mkoani hapa wanaendesha msako mkubwa.By.BBC

No comments:

Post a Comment