header

nmb

nmb

Sunday, May 9, 2010

TANGAZO....AKUDO KUPEKECHAPEKECHA JIJINI!!


Bendi ya Akudo Impact yenye maskani yake Jijini dar es salaa inataraji kufanya onyesho moja maalum Mkoani Iringa kwa ajili ya kutambulisha nyimbo zake mbili ilizozirekodi na kuzisambaza vituo mbalimbali vya redio hivi karibuni.
Kwa mujibu wa muandaaji wa onyesho hilo Issa Mwendapole amesema Bendi hiyo inatarajiwa kufanya onyesho hilo siku ya jumatano tarehe 19 mwezi huu wa tano katika club maarufu mkoani Iringa inayoitwa VIP kuanzia saa mbili za usiku.
Aidha Mwendapole ameendelea kusema ya kuwa matayarisho yote kwa ajili ya onyesho hilo yamefikia hatua nzuri na Bendi ya Akudo Impact imejitayarisha vilivyo ili kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa dansi watakaohudhuria onyesho hilo.
"Bendi inatarajiwa kuwasili siku ya Jumatano tarehe 19 asubuhi tayari kabisa kwa ajili ya kutoa burudani usiku wake na uongozi wa Akudo umenihakikishia kuleta wanamuziki wake wote nyota watakaoongozwa na Rais wao Christiant Bella, Kaimu Rais Tarsis Masella, waimbaji Zagreb Butamu na Allain Kabaselle."
Nyimbo wanazotaraji kuzitambulisha ni "ubinafsi" uliotungwa na Tarsis Masella na ''Pongezi kwa wana ndoa" uliotungwa na Bella aidha wana rapu zao mpya pamoja na shoo kali zitakazo nakshiwa na wanenguaji wao wapya waliowatoa Kongo.
Natoa wito kwa wakazi wa iringa wajitokeze kwa wingi ili kuja kupata Burudani ambayo huwa inapatikana mara chache Mkoani Iringa."Mara ya mwisho Akudo walipita Mkoani Iringa mwishoni mwa mwaka jana na walipiga ukumbini hapo hapo VIP mashabiki walijitokeza kwa wingi hivyo tunawasihi mashabiki wajitokeze kwa wingi kama walivyojitokeza mwaka uliopita" alimaliza kusema mwandaaji huyo.

No comments:

Post a Comment