header

nmb

nmb

Saturday, May 8, 2010

SIMBA WAOMBA WATANZANIA KUWAOMBEA WADAI WAKO FITI!!

Wachezaji wa Simba wakibeba mabegi
katika picha ya pamoja na wadau waliokwenda nchini Misri

Wachezaji wa simba wakishusha mizigo yao mara baada ya kuwasili jijini Alexandria kwa basi wakitokea jijini Cairo walikokuwa wamepiga kambi katika hoteli ya Nile Paradise Inn Cairo. ili kujiandaa na mchezo wa kombe la Shirikisho la Afrika CAF dhidi ya timu ya Kharas El Hadood ya huko.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kesho ambapo katika mchezo wa awali uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Simba ilifanikiwa kuifunga Haras El Hadood magoli 2-1.

Katika mchezo huo Simba inahitaji kushinda au Sare ya aina yoyote ili iweze kusonga mbele katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika baada ya ili ya klabu bingwa.

MWENYEKITI wa kamati nya usajili wa klabu ya Siumba Kassim Dewji,amesema ana uhakika wachezaji wake kuibuka kidedea katika mchezo wa kesho na dhidi ya Haras El Hadood kama walivyofanya kwa Zamalek.Akizungumza jana Dewji amesema kuwa ana uhakika wa kuibuka wachezaji hao watarudisha historia hiyo katika mchezo huo utakaochezwa kesho kuanzia saa 1.30 mjini Alexandria.
Dewji alisema ana kila sababu ya kufanya hivyo kutokana na maandalizui mazuriu waliyowapa wachezaji wake wakiwa nchini hapa.Alisema kwa ujumla amesikia furaha kuoina yupo karibu sana na watu wa Ubalozi kwa kushirikiana nao katika kila jambo ambalo.
Dewji alisema kuwepo kwa wachezaji wake mapema nchini hapa kumewaongezea ari kubwa hivyo ni matumaini yake watawapa furaha watanzania.“Tumefarijika sana kuona tupo karibu na ubalozi unatusaia kwa kila jambo tuna matumaini ya kufanya makubwa katika mchezo huo na kukumbusha ya mwaka 2003 tuliwatoa mabingwa wa Afrika katika mashindano”alisema Dewji.Tanzania matumaini yake wachezaji wake watagapigana kufa na kupona kuhakikisha wanaibuka washindi katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment