header

nmb

nmb

Saturday, May 8, 2010

MAMBO YA WIKIENDI HII TUNA ZUNGUMZIA KUCHA!!




WENGI hawafahamu aina ya kucha walizonazo, na hii huwagharimu wakati wa kuzitengeneza kwa kutumia vifaa ambavyo si sahihi.
Matumizi ya vifaa ambavyo si sahihi, na mazingira husababisha kucha kukosa afya, pia kuharibu shepu yake ya awali kutokana na shughuli za kila siku katika maisha ya binadamu yeyote, hivyo ni vyema kuzikinga kucha zako na maradhi kwa kuzifanyia usafi kila siku au mara kadhaa kwa wiki ili kuzilinda.

Kuna wengine wanakucha ngumu, laini na ambazo zipo wastani, usitumie kifaa cha kucha ngumu kwa kucha laini au kifaa cha kucha laini kwa kucha ngumu.

Ni vyema kama unajali, kutumia muda mwingi kuzifuatilia kucha zako na kuelekeza nguvu katika kuhakikisha zinakuwa katika matunzo mazuri na kujitahidi kubuni mtindo ambao unaweza kuwa tofauti na wengine.

Hata hivyo, ili uwe na kucha nzuri zenye mvuto unatakiwa kunywa maji mengi kila siku ili kupata afya ya kucha zako pamoja na mahitaji mengine mengi katika mwili wako vikiwemo vyakula vyenye vitamini nyingi.

Katika kutunza kucha ziwe nzuri, vyakula ambavyo ni mlo kamili ni muhimu sana. Kucha ni kiungo kidogo lakini kina thamani na umuhimu mkubwa katika suala zima la urembo.

No comments:

Post a Comment