header

nmb

nmb

Thursday, May 6, 2010

Rais wa Nigeria afariki dunia!!

HAYATI UMARU YAR'ADUA ENZI ZA UHAI WAKE

RAIS Nigeria, Umaru Yar'Adua (58), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kutokana na tatizo la moyo lililokuwa likimsumbua kwa muda mrefu.

Aliyekuwa Rais wa muda katika kipindi chote cha matibabu ya Yar'Adua, Goodluck Jonathan, ataendelea kushikilia kiti hicho mpama hapo taratibu zingine zitakapotangazwa.

Uchaguzi wa nchi hiyo kulingana na kanuni iliyojiwekea unatarajiwa kufanyika April 2011 ambapo ndio kipindi cha kwanza cha Yar'Adua kilitarajiwa kumalizika.

“Nigeria imepoteza kiongozi shupavu hasa katika kipindi kama hiki,” amesema Jonathan na kutangaza siku saba za maombolezo nchini humo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti.

Mazishi ya Yar'Adua yanatarajia kufanyika leo jioni kusini mwa Mji wa Katsinaatika.

Waziri wa Habari nchini humo Dora Akunyili amesema Yar'Adua amefarikia usiku wa kuamkia leo.

Rais wa Marekani, Barack Obama, ametuma salamu za rambirambi kwa wananchi wa Nigeria.

Obama amemtaja Yar'Adua kuwa alikuwa rai makini na mwenye upeo mkubwa katika kujua na kutatua matatizo ya wananchi wake licha ya kuandamwa na maradhi kwa kipindi kirefu.BBC

No comments:

Post a Comment