header

nmb

nmb

Thursday, May 6, 2010

MISS Arusha City Centy Maandalizi yaiva

Wanyagi wa kitongoji cha Arusha wakijifua tayali kwa Mashindano
Mkurugenzi wa Sophy Entertainment, Sophia Urio akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliyofanyika jana jioni jijini Arusha. Kutoka kulia ni Henry Tzamburakis ambaye ni meneja wa Vodacom Kanda ya kaskazini, Beatrice Dallaris ambaye ni meneja wa hoteli ya Naura Springs,
Wengine ni Nsia Swai ambaye ni mmoja ya majaji na Daniford Mpumilwa ambaye ni jaji mkuu katika shindano hilo.


Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Eng. Raymond Mushi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kinyang’anyiro cha Vodacom Miss Arusha City Center inayofanyika kesho katika ukumbi wa hoteli ya Naura Springs.Akifafanua katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi huo, Mkurugenzi wa Sophy Entertainment, Sophia Urio ambao ni waandaaji wa kinyang’anyiro hicho alisema kuwa kwa sasa wamejipanga vyema.
“Tunashukuru sana waandishi wa habari ambao wamekuwa bega kwa bega na sisi katika kufanikisha hilo ambalo linatarajiwa kuanza kesho saa 1 usiku na kumalizika saa 6 usiku.Kampuni yetu ndiyo ya kwanza kwa mkoa wa Arusha kufungua mashindano ya Vocodacom Miss Arusha City Center na kufuatiwa na vitongoji vingine.“Tunamshukuru Mungu tumepata washiriki wenye mvuto mbele ya jamii na tunaamini shindano letu litakuwa na ushindani na msisimo”. Alisema Sophia”.Kwa sasa tunao warembo 11 hao wapo kambini wakijinoa tayari kujiandaa kwa ajili ya mashindano hayo.
Mataji yatakavyoshindaniwa ni Vodacom Miss Arusha City Center na Balozi wa Naura Springs Hotel.
Wasanii watakaotumbuiza katika onyesho hilo ni Kikundi cha ngoma za asili kiitwacho Perfect Youth Group, Bendi iitwayo Aqua Sound na wasanii wengine ni Hussein Machozi huyu ni msanii wa hapa Tanzania.Tunawashukuru sana wadhamini wetu ambao ni Vodacom, Naura Spring Hotel, Little Roses, Aqua Sound, Shuphaa Quality Boutique, Janneth Beauty Parlour.By Said Njuki Arusha

No comments:

Post a Comment