header

nmb

nmb

Wednesday, May 26, 2010

MAUWAJI YA WANAWAKE YANAENDELEA

Na Benedict Kaguo, Tanga
MKAZI wa Kijiji cha Mgwashi Kata ya Bumbuli wilayani Lushoto Mkoani Tanga ameuwawakikatili kwa mumewe kwa kukatwa shingo kwa panga na mumewe kwa kile kilichodaiwa ni mfarakano katika ndoa yao.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Mei 20 mwaka huu, saa moja asubuhi katika kijiji hicho baada ya mumewe Frank Festo (35) kudaiwa kugombana na mkewe na kuamua kufanya ukatili huo. Tukio hilo lilivuta hisia kali kwa wakazi wa kijiji hicho linahusishwa na wivu wa kimapenzi ambapo kabla ya kutokea tukio hilo, mtuhumiwa huyo alikwenda nyumbani kwa wazazi wa marehemu kushtaki juu ya mgogoro wa ndoa yao.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabasi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kumtaja aliyeuwawa kuwa ni
Magreti Frank (34) ambaye ni mkazi wa kijiji hicho.
Kamanda Sabasi alisema tukio hilo lihahusishwa na mgogoro wa kifamilia ambapo awali mtuhumiwa huyo alikwenda kuripoti kwa wakwe zake.
Amesema kuwa tayari Jeshi la Polisi mkoani Tanga limefanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo ambapo baada ya kukamilika kwa uchunguzi atafikishwa Mahakamani.

No comments:

Post a Comment